• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Azindua Utoaji wa Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi Mkoani Simiyu

Posted on: April 25th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amezindua rasmi leo zoezi la chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi ambayo inatarajiwa kutolewa kwa watoto wa kike takribani 37,141 wenye umri wa miaka 14 kwa mkoa mzima wa Simiyu.

Uzinduzi huo umefanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Sima A na Sima B na kushirikisha watoto wenye umri wa miaka 14 kutoka katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari za Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Akizungumza na wanafunzi walioshiriki katika uzinduzi wa chanjo hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wa kuwahamasisha wenzao kwenda kupata chanjo na kuwahamasisha wazazi kuwahimiza watoto wa kike wote wenye umri wa miaka 14 kwenda kupata chanjo hiyo.

Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Simiyu Bibi.Beatrice Kapufi ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wenye umri wa miaka 14, wanapata haki yao ya kupata chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi ambayo itatolewa bila malipo katika vituo vya kutolea huduma za afya, shule za Msingi na Sekondari.

Aidha, amesema Mkoa kupitia Kitengo cha Huduma za Chanjo wameshatoa mafunzo kwa watendaji, watoa huduma wote wa vituo vinavyotoa huduma ya chanjo na walimu wanaojishughulisha na huduma za Afya katika Shule za Msingi na Sekondari zote mkoani Simiyu.

“Nitoe wito kwa wazazi wote kuhakikisha watoto wa kike wote wenye miaka 14 wanapata haki yao msingi kupata chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi, chanjo hii inatolewa bure na itatolewa mara mbili, mtoto akishapata kwa mara ya kwanza atatakiwa kwenda kupata chanjo ya pili baada ya miezi sita” alisema Kapufi.

Nao wanafunzi waliopata chanjo wameishukuru Serikali kwa kuwaletea chanjo hiyo ambayo wamesema itawasaidia kujikinga na maambukizi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi.

“Tunashukuru sana Serikali kwa kutuletea chanjo hii itatusaidia tusipate Saratani ya Mlango wa Kizazi, nawaomba wazazi wawaambie wenzetu nao waende wakapate chanjo hiyo, ili wasipate Saratani wakiwa wakubwa” alisema Flora Masunga mwanafunzi wa Shule ya Msingi Sima B.

MWISHO

KUPATA HABARI KAMILI KUHUSU HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/04/rc-mtaka-azindua-rasmi-utoaji-wa-chanjo.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa