• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Awataka Wananchi, Viongozi Simiyu Kutoa Ushirikiano Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya

Posted on: March 1st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi na Viongozi Mkoani humo kutoa ushirikiano kwa wadadisi na wataalam wa Takwimu katika utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi unaoendelea hapa nchini ili kuwezesha upatikanaji wa  takwimu halisi na sahihi Mkoani humo.

Mtaka ameyasema hayo katika Mkutano wake na   waandishi wa habari, wataalam wa Takwimu na Viongozi wa madhehebu ya dini uliofanyika Februari 28 Mjini Bariadi.

Amesema Utafiti huo utatoa makadirio ya uchumi jumla(macroeconomic), hususani matumizi ya kaya kwa ajili ya Pato la Taifa (Gross Domestic Product-GDP), kupata mwenendo wa matumizi ya moja kwa moja ya kaya  ili kuwezesha uchambuzi wa hali ya soko na kupata taarifa za umilikaji wa vifaa vya kudumu pamoja na nyenzo za uzalishaji wa kipato.

Amesema kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2015 kila mwananchi anawajibika kushiriki katika utafiti kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu rasmi ambazo zitatumika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.

“ Lengo mama la utafiti huu ni kujua hali ya kipato kwa kaya zetu asije mtu akapotosha kuwa watafiti wana agenda nyingine, ndiyo maana nimeona viongozi wa Dini nao walifahamu hili ili wasaidie kuwaeleza kwa ufasaha waumini wao; Serikali inahitaji takwimu sahihi ili ipange bajeti  na kuweka mipango ya maendeleo, niwaombe wananchi na viongozi tutoe  ushirikiano” alisema Mtaka.

Aidha, amemuagiza Meneja wa Takwimu mkoani humo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ushiriki wao katika utafiti huu hususani kaya zilizochaguliwa na akamtaka yeye na wataalam wa Takwimu wa Mkoa huo kufanya mikutano katika minada na magulio pamoja na maeneo ya yenye idadi kubwa ya watu yakiwemo ya Makao Makuu ya Wilaya na miji midogo(centers) ili kujenga uelewa kwa wananchi.

Meneja wa Takwimu Mkoa wa Simiyu, Nestory Mazinza amesema tangu utafiti huu uanzae Desemba Mosi 2017 jumla ya kaya 102 zimeshafanyiwa utafiti kati ya 408 zinazotarajiwa kufikiwa mpaka kumalizika kwa zoezi hilo mwezi Novemba  2018.

Naye Bi.Joyce Luhende Mdadisi kutoka Wilaya ya Meatu amesema wanapofanya utafiti huu wanakutana na changamoto mbalimbali na kubwa ikiwa ni baadhi ya wanakaya kuogopa kutoa taarifa zinazohitajika wakati wakihojiwa hali inayopelekea kukosekana kwa taarifa sahihi.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Dini, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikiristo Tanzania(CCT) Mkoa wa Simiyu, Mchungaji Martine Samson Nketo amesema kupitia ibada  watasaidia kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utafiti huu na kuwaeleza umuhimu wake katika mipango ya maendeleo inayopangwa na Serikali.

  Kaya zilizochaguliwa k kufanyiwa utafiti huu zinatoka katika maeneo 34 (Vijiji/Mitaa) kwenye Wilaya zote tano za Mkoa wa Simiyu yaliyopo katika kata za Nkindwabiye, Nyangokolwa, Sakwe, Nyakabindi, Dutwa, Matongo,Gilya, Sima,Mwamtani, Mwaswale, Mwamapalala, Nhobora, Zagayu, Kinang’eli, Mwanhuzi, Mwandoya, Sakasaka, Mwabuma, Lubiga, Ng’oboko, Busilili, Seng’wa, Masela, Mwamashimba, Buchambi, Badi, Nyalikungu, Kiloleli,Kalemela, Mkula na Ngasamo.

MWISHO

KUPATA  PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/03/rc-mtaka-awataka-wananchi-viongozi.html

 

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa