Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa Wafanyabiashara wazawa kuwekeza katika mkoa huo na kuwahakikishia kuwa Serikali iko tayari kuwaunga mkono.Mtaka amesema hayo katika ufunguzi wa Jukwaa la biashara lililofanyika leo mjini Bariadi, ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali(TSN) ikishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Amesema fursa takribani 14 zimetangazwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo baada ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) uliopelekea kuandaliwa kwa Rasimu ya mwongozo wa uwekezaji wa mkoa.
"Tunataka kutransform mkoa wa Simiyu na kuufanya kuwa wa tofauti katika kuelekea kwenye uchumi wa kati, Tungehitaji kujenga mkoa tofauti na watu wengine waje wajifunze; yapo tuliyoanza kutekeleza na yapo yaliyo kwenye pipeline" alisema.
Mtaka amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo, kutoweka urasimu usio wa lazima kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika maeneo yao.Ameongeza kuwa mkoa wa Simiyu umeanzisha mfumo tofauti wa kushirikisha Sekta binafsi katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda ambapo wameanza kwa Halmashauri kuendesha viwanda vidogo kwa ubia na Vikundi vya Vijana; Wilaya ya Meatu(kiwanda cha kusindika maziwa) na Wilaya ya Maswa (Kiwanda cha kutengeneza Chaki).Aidha, pamoja na kuwepo kwa viwanda vidogo Mtaka amesema Serikali mkoani Simiyu imedhamiria kuwa na viwanda vya kati na vikubwa kwa lengo la kuyaongezea thamani mazao ya kilimo na mifugo.Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, ambaye pia ni Mtaalam wa masuala ya biashara, Profesa Elisante Ole Gabriel amewataka wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari ili biashara zao ziwe endelevu.
Pia Profesa Ole Gabriel ametoa rai kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu kuzijua vema biashara zao na kufanya biashara hizo kimkakati hususani katika kubuni biashara zinazojibu changamoto za jamii na suala la huduma bora kwa wateja.Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Ndg.Richard Kayombo ametoa wito kwa wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara zao ili walipe kodi kulingana mapato yao ili kuiwezesha serikali kupata kodi/mapato stahiki.Naye Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali(TSN) ambao ndiyo waandaaji wa Jukwaa la biashara, Dkt. Jim Yonazi amesema wao wanaamini maendeleo ni Habari, hivyo wako tayari kufanya kazi na mkoa wa Simiyu kwa kuwa viongozi wake wanachukia kasi ndogo katika maendeleo.
"Wakati wengine wanaona Simiyu kama mkoa mpya sisi tunaona fursa, tumeamua kupeleka habari za uwekezaji na maendeleo ya mkoa huu sehemu mbalimbali duniani kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na sasa hivi watu zaidi ya 80,000 wanajua nini kinaendelea hapa" alisema.Jukwaa la biashara mkoani Simiyu limeandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) yaani Habari Leo, Daily News na Spoti Leo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Wadau wengine ni Benki ya Maendeleo(TIB), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Benki ya NMB na Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC).Jukwaa hilo limewahusisha viongozi wa Mkoa huo ngazi ya Mkoa na Wilaya, wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa Maendeleo wa Mkoa huo.