• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Atoa Wito kwa Wananchi Kujitokeza Kwa Wingi Maonesho Ya Sido Kitaifa Simiyu

Posted on: October 21st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi mkoani humo na maeneo mengine nchini kujitokeza kwa wingi kushirikia katika  Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23-28, mwaka huu katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani humo na kubainisha kuwa Maandalizi yote yamekamilika.

.Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mtaka amesema Maonesho haya yatafunguliwa rasmi siku ya Jumanne Oktoba 23, 2018 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.

Ameongeza kuwa katika maonesho hayo wajasiriamali, waoneshaji wa teknolojia mbalimbali wamealikwa na kusisitiza kuwa hii ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine kuona ushindani katika uongezaji wa thamani wa mazao mbalimbali na fursa kwa wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wenzao.

“ Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu kujitokeza kushiriki maonesho haya maana hii ni fursa kwao ya kuweza kujielimisha katika maeneo mbalimbali ya teknolojia za viwanda hususani viwanda vidogo, lakini pia wajasiriamali watapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa maeneo mengine nchini na nje ya nchi” alisema Mtaka.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji wa  Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Shoma Kibende amesema tayari wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali wamethibitisha kushiriki maonesho hayo na baadhi yao wameanza kuwasili.

“Wajasiriamali zaidi ya 1000 kutoka mikoa yote nchini wanatarajia kushiriki maonesho haya na baadhi yao wameshaanza kuwasili, lakini pia kuna taasisi mbalimbali ambazo ni taasisi shirikishi na SIDO, huduma za kupata ubora hii ni fursa pekee kwa Watanzania” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe amesema zaidi ya wajasiriamali 51 kutoka wilayani humo watashiriki katika kuonesha bidhaa mbalimbali ambazo wametengeneza na kuzalisha kupitia viwanda vidogo.

Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Kagera,Richard Mahela amesema maonesho ya SIDO ambayo ni ya kwanza kufanyika Kitaifa  yatawasaidia wajasiriamali kote nchini kupanua masoko ya bidhaa zao kwa kuwa wameandaa vipeperushi vya bidhaa zao ambavyo  vitasambazwa kwa lengo la kusaidia kuwaunganisha na wanunuzi.

Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa ambayo ni ya kwanza kufanyika ngazi ya Kitaifa yatafunguliwa rasmi Jumanne Oktoba 23, 2018 na kuhitimishwa siku ya Jumapili Oktoba 28, 2018 yakiwa na Kauli Mbiu: PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI”.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/10/rc-mtaka-atoa-wito-kwa-wananchi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa