• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Atoa Wito kwa Jamii kushiriki Vita Dhidi ya Mimba kwa Wanafunzi

Posted on: March 14th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wazazi, walimu na watumishi wengine wa Serikali, wanafunzi wa kike wanaopata mimba na jamii yote kwa ujumla kushirikiana na Serikali kuhakikisha wale wote waliowapa mimba wanafunzi wanabainika na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mtaka ameyasema hayo wakati akifunga kikao kazi cha viongozi na watendaji wa idara ya elimu kilichofanyika Machi 12, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha taaluma mkoa wa Simiyu.

Amesema katika uchunguzi wa awali uliofanyika imebainika kuwa wazazi, walimu, Maafisa Watendaji wa Kata na watumishi wengine wa Serikali na wanafunzi wenyewe waliopewa mimba wamekuwa wakikwamisha juhudi za serikali katika vita hii kwa kuwa sehemu ya kuharibu ushahidi.

“Kuna mimba zaidi ya 300 zimripotiwa katika maeneo mbalimbali baadhi ya maeneo wazazi wanashiriki kuharibu na wakati mwingine wanafunzi waliopata mimba wanashirikina na wazazi kuharibu ushahidi wa kesi wasi za wanafunzi wajawazito, baadhi ya maeneo walimu wetu wamehisiwa, kwingine watendaji wetu, naomba tushirikiane kuwabaini watu wanaowapa wanafunzi mimba kwenda  kwenye hatua” alisema Mtaka..

Ameongeza kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa imekaa na wameshakubaliana hatua za kuchukua kwa wanafunzi, watumishi, wazazi na watu wote waliokatisha ndoto za wanafunzi wa kike kwa kuwapa mimba.

Kwa  upande wake Mwalimu  Huruma Mjinja kutoka Shule ya Sekondari Kidinda, amesema katika kukabiliana na tatizo la mimba kwa wanafunzi ni vema walimu na wazazi wakashirikiana kuwalinda watoto wa kike na wapate muda wa kuzungumza nao.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka amesema Wanafuzi wa kidato cha sita mkoani hapa wanatarajia kuanza kambi za kitaaluma rasmi Machi 31, 2019 kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa Taifa.

Aidha, Mtaka amewataka Wakuu wa shule za sekondari zenye wanafunzi wa kidato cha nne chini ya 25 kukutana na wazazi ili wakae na kukubaliana baadaye  kuwakusanya wanafunzi hao kwa pamoja katika Shule ya sekondari Simiyu kwa ajili ya kufanya kambi za kitaaluma.

“Tunamaliza kujenga Simiyu Sekondari tukiwa na ziada ya vyumba vya madarasa 20 hivyo wakikaa watu 40 kwa kila chumba ni wanafunzi 800 tunajenga mabweni manne; shule zote za sekondari zenye wanafunzi wa kidato cha nne chini ya 25, bodi zao na viongozi wa Serikali wakae pamoja shuleni hapo kwa ajili ya kambi za kitaaluma baada ya likizo ya MweziAprili, 2019” alisema Mtaka.

Nao Baadhi ya Wakuu waShule wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanafanya vizuri ili mkoa uweze kufanya vizuri pia kitaaluma huku akiomba viongozi wa mkoa waendelee kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vvizuri ili waweze kufanya vizuri zaidi kila mwaka.

“ Tutafanya jitihada kuhakikisha tunafanya vizuri lakini tunaomba viongozi wetu waendelee kuona haja ya kutoa motisha kwa wanaofanya vizuri kwa sababu mkiendelea kufanya hivyo mtatupa nguvu ya kufanya vizuri zaidi” Mwalimu Enelico Mwandibila kutoka wilaya ya Itilima.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema mkoa huo umejiweka mkakati kabambe wa kuimarisha ufuatiliaji na ufundishaji na tathmini itafanyika kila mwezi kujua vipindi vilivyofundishwa na ambavyo havijafundishwa vitafidiwa.

Kikao hiki kimehudhuriwa na Maafisa Elimu na Taaluma wa Mkoa na Wilaya, baadhi ya Waratibu Elimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari za Kidato cha Nne, wadhibiti ubora na baadhi ya wadau wa elimu mkoani Simiyu.

MWISHO.

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/03/rc-mtaka-atoa-wito-kwa-jamii-kushiriki.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa