• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Rc Mtaka apongeza jeshi la polisi kupunguza matukio ya uhalifu

Posted on: April 27th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa kupunguza matukio ya uhalifu hali iliyobadili taswira ya mkoa na kuufanya usikike katika masuala  maendeleo.

Mtaka ametoa pongezi hizo katika kikao chake na Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani humo kilichofanyika leo  Mjini Bariadi.

Amesema askari wa Jeshi la Polisi wamefanya kazi kubwa katika kubadili taswira ya mkoa wa Simiyu ambapo kwa sasa viongozi na wananchi wamekuwa wakijadili masuala ya maendeleo ukiwemo Uchumi wa Viwanda kwa sababu ya amani na utulivu uliopo.

“Simiyu ya zamani ni tofauti kabisa na ya sasa,  zamani tulikuwa tukiangalia TV, tukisikiliza redio au kusoma magazeti habari zilikuwa ni mauaji ya vikongwe, kukatana mapanga na mauaji ya watu wenye ualbino.  Pamoja na viongozi wa Dini kuomba Mungu kwa ajili ya mkoa wetu lakini Jeshi la polisi pia limefanya kazi kwa nafasi yake pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama ” alisema Mtaka.

 Aidha, amesema Serikali imedhamiria kuujenga Mkoa wa Simiyu kuwa Mkoa mpya wa kiuchumi jambo ambalo linapaswa kujulikana na wadau wote muhimu wa maendeleo wakiwemo viongozi na askari wa Jeshi la Polisi ambao aliwataka kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji na maendeleo mkoani humo.

“ Chini ya Falsafa ya Wilaya Moja Bidhaa Moja, Sasa hivi Maswa wanatengeneza chaki, Meatu wanasindika Maziwa na tunapanua kiwanda cha maziwa kwa kufanya uwekezaji mkubwa ambapo pia tutatengeneza maziwa ya unga kwa ajili ya watoto, tutaanza kilimo cha umwagiliaji Busega pamoja na kuanzisha kiwanda cha kutengeneza Tomato sauce; hapa kila wilaya ina jambo la kufanya, hizi zote ni fursa  ninyi askari na viongozi changamkieni fursa zilizopo” alisisitiza.

Ameongeza kuwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, Mkoa wa Simiyu unatarajia kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje kwa asilimia 40%  kwa kuwa vitaanzishwa viwanda vya kuchakata mazao mbalimbali yanayopatikana hapa nchini katika kilimo, mifugo na uvuvi.

Wakati huo huo Mtaka amewataka askari wa jeshi la polisi kutekeleza majukumu kwa kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kupima nguvu ya kutumia kukabiliana na raia katika matukio mbalimbali na kuepuka fedheha ya kuwa watoa taarifa kwa wahalifu.

Vile vile amewataka askari wote kuwa waangalifu katika lugha wanayotumia wakati wakiwa wanatekeleza majukumu yao.

Wakati akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mkoa kwa nasaha mbalimbali alizotoa kwa Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Boniventure Mshongi amewataka viongozi na askari kufanya kazi zao kwa weledi huku wakizingatia maadili yao.

Katika kikao hicho viongozi na askari wa Jeshi la Polisi wamewasilisha maoni, mapendekezo na maombi mbalimbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ikiwa ni pamoja na kuomba Mamlaka za Serikali za Mitaa kupima na kuwauzia viwanja kwa bei nafuu ili wajenge na kuendeleza Mkoa huo.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa