• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Apiga Marufuku Ushuru wa Biashara Ndogondogo Maarufu kama Matandiko

Posted on: September 5th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amepiga marufuku Halmashauri zote Mkoani humo kutoza ushuru wa biashara ndogondogo zinazofanywa na wananchi kwa kutandika na kupanga bidhaa zao chini au kuuzwa katika mabeseni maarufu kama matandiko.

Mtaka ametoa agizo hilo baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Igaganulwa, Mhe.Nhandi Masaka Kachala na baadhi ya wananchi kutoa malalamiko yao kuhusu ushuru huo, wakati wa ziara yake wilayani Bariadi yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi .

Amesema suala hilo lilishatolewa maelekezo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, hivyo Halmashauri zinapaswa kubuni vyanzo vipya vya mapato vyenye tija kwa Halmashauri na wananchi badala ya kutegemea kutoza ushuru unaowakwaza wananchi.

“Kama kuna Halmashauri bado inatoza ushuru wa matandiko wamechelewa sana, kuanzia kesho hamna huo ushuru, kama ninyi mnafikiri mapato ni kutoza tandiko la nyanya, dagaa, mchicha na ninyi  kama wakuu wa idara hiki ndicho chanzo mnachokifikiria kichwani hiyo kazi haiwafai, mkatafute kazi nyingine ya kufanya” alisema Mtaka.

 “Halmashauri lazima ibuni chanzo cha mapato chenye tija kwenye Halmashauri na watu. Sasa mtu anahangaika na beseni lake la nyanya wewe unamtoza ushuru, umechangia nini, beseni si lako nyanya si zako” alisema Mtaka.

Aidha, ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi  kuhakikisha kuwa inarejesha asilimia Kumi ya mapato yanayokusanywa inayokusanywa kutoka katika vijiji vyote kwenye kila robo mwaka ili Vijiji hivyo viweze kutekeleza mipango ya maendeleo iliyowekwa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewahamasisha wananchi kuendelea kulima pamba kwa kuwa Serikali imekusudia kujenga kiwanda cha bidhaa ya Afya zitokanazo na zao la pamba mkoani humo na wataalam wanaofanya upembuzi yakinifu wanatarajia kufika Mkoani Simiyu Septemba 20 mwaka huu kuja kuona eneo kitakapojengwa kiwanda.

Amesema wananchi wasikate tamaa kulima pamba kwa sababu ya matatizo ya kihistoria na kuwaeleza kuwa, Serikali ya Mkoa imepanga mikakati madhubuti ya kuirudisha pamba kuwa dhahabu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata mbegu bora, dawa, pembejeo zote na suala la bei ya pamba itaanza kujadiliwa mapema.

Ameongeza kuwa wananchi wasiache kulima mazao jamii ya mikunde hususani choroko na dengu kwa kuwa Serikali inashughulikia suala la upatikanaji wa soko la uhakiki pamoja na kupunguza au kuondoa kabisa  madalali katika biashara ya mazao hayo ili wananchi wanufaike kupitia kilimo.

Akitolea ufafanuzi hoja ya Diwani wa Kata ya Ikungulyabashashi Mhe.Bupi Maduhu Litunga ya kupimiwa maeneo, Mkuu wa Mkoa huyo wa Mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi kupitia Idara ya Ardhi, kuitisha mikutano katika Vijiji vyote ambavyo wananchi wanahitaji  kupimiwa maeneo na baadae awasilishe mihutasari ya vikao hivyo Ofisini kwake tarehe 13/09/2017.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amekamilisha ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ambapo amesikiliza na kutatua kero za wananchi katika sekta ya Elimu,Afya, Kilimo, Mifugo, Ardhi, Ujenzi, Biashara na Uchumi pamoja na suala la utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA) ambazo amezitolea maelekezo na ameahidi kufuatilia utekelezaji wake.


.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga  akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa  wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  aliyofanya  Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi

Diwani wa Kata ya Dutwa Wilayani Bariadi, Mhe.Mapolu Nunde Mkingwa akizungumza na wananchi wa Kata hiyo (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa  wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  aliyofanya  Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mpina Nkwabi Mkazi wa Dutwa Wilayani Bariadi akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa ziara yake wilayani humo yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Dutwa wakimsikiliza wilayani Bariadi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa