Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MHE. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo pia ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini, ili kuiwezesha Bohari ya Dawa (MSD) ambayo ni mzabuni wa dawa na vifaa tiba wa nchi za SADC kupunguza uagizaji wa dawa na vifaa tiba nje ya nchi.
Mtaka ametoa pongezi hizo Agosti 21, 2019 wakati akifunga mkutano wa siku tatu wa Menejimenti ya Bohari ya Dawa (MSD) na mameneja wa Kanda za Bohari ya Dawa (MSD) uliofanyika kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji.
Mtaka amesema Bohari ya Dawa kama mzabuni wa dawa na vifaa tiba katika nchi za SADC wanapaswa kutumia fursa ya Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kuhimiza wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba.
“Nampongeza Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na Pongezi nzuri kwa Mhe. Rasi ni pale ambapo nchi yetu ambao pia tuna faida ya kuwa mzabuni wa dawa na vifaa tiba kwenye SADC; tutapata Watanzania wengi watakaochangamkia fursa ya kuwekeza na kutumia nafasi ya Tanzania kuwa Mwenyekiti wa SADC tukiwa na Idadi ya watu wengi kwenye soko la dawa na vifaa tiba” alisema Mtaka.
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/08/mkuuwa-mkoa-wa-simiyu-mhe.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa