Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry
Katika mazungumzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Jumuiya hiyo kwa namna ilivyowekeza katika miradi ya mbalimbali ikiwemo miradi ya maji hususani uchimbaji wa visima katika baadhi ya maeneo mkoani humo.
Aidha, ameiomba Jumuiya hiyo kuona uwezekano wa kuwekeza kwenye sekta ya Afya hasa katika ujenzi wa Hospitali huku akiwahakikishia upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya ujenzi pindi watakapokuwa tayari.
Kwa upande wake Kiongozi Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema atalichukua kama pendekezo kwa viongozi wenzake ili waweze kuona uwezekano wa kuwekeza katika ujenzi wa hospitali Mkoani Simiyu.
Wakati huo huo Kiongozi huyo amesema pamoja na kuchimba visima vya maji Jumuiya ya Ahmadiyya imewekeza katika Elimu na Afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Naye Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Mkoa wa Simiyu, Shekh Abdulatif Yusuph Ngalombe amesema hadi sasa jumuiya hiyo imechimba visima 6 katika wilaya ya Itilima na kuboresha visima 19 katika wilaya ya Itilima na Meatu kwa gharama ya shilingi 49,760,000 na kazi ikiwa bado inaendelea katika baadhi ya maeneo.
KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI NI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/07/rc-mtaka-akutana-na-kiongozi-wa-jumuiya.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa