• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Aishauri TFDA kufungua Ofisi katika Mikoa

Posted on: May 24th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameishauri Mamlaka ya Chakula na Dawa hapa nchini (TFDA) kufungua Ofisi katika Mikoa ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza ufanisi hususani katika kipindi hiki ambacho Serikali ya awamu ya Tano inahimiza utekelezaji wa ajenda ya Viwanda.

Mtaka ameyasema hayo Mei 23 wakati akifungua kikao kazi cha Wahariri na waandishi wa habari wa mikoa ya Simiyu na Mara kilicholenga kuhamasisha Sheria ya Chakula, dawa na vipodozi sura Na.219, ambacho kilifanyika Mjini Bariadi.

Amesema wakati huu ambao Sera ya Viwanda ni kipaumbele cha nchi ni vema Ofisi za TFDA zikawepo katika kila Makao Makuu ya  mkoa ili pale watu wanapotaka kujenga viwanda vitakavyozalishwa dawa, chakula na vipodozi waweze kupata huduma zinazotakiwa kwa wakati badala ya kufuata huduma katika ofisi za kanda.

“Mhe. Rais anapohimiza ajenda ya viwanda kwenye nchi TFDA inabidi ione umuhimu wa kuwa na Ofisi kwenye mikoa, ili mfano watu wa Simiyu wanapohitaji kufungua kiwanda cha bidhaa ambazo zinaihusu TFDA wasilazimike kwenda Mwanza kufauta huduma” alisema.

 

Aidha, Mtaka ameishauri Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini - TFDA kutoa ufafanuzi wa mara kwa mara kuhusu dawa, chakula na vipodozi kupitia vyombo vya habari, ili jamii iweze kuwa na uelewa mpana wa madhara yatokanayo matumizi na bidhaa bandia na zenye madhara kwa binadamu.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa waandishi wa habari baada ya kupata mafunzo kutoka TFDA kuwa mabalozi  wazuri wa TFDA katika kufafanua masuala yote yenye sintofahamu na kuandika habari za kiuchunguzi zilizofanyiwa utafiti kuhusu dawa, chakula na vipodozi.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi Agnes Sitta Kijo amewataka Waandishi wa habari kutoa taarifa pale wanapobaini uwepo bidhaa ambazo si salama kwa matumizi ya binadamu huku akiwasisitiza kujikita katika uandishi wa Habari za kiuchunguzi.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho kutoka Mikoa ya Simiyu na Mara wamesema mafuzo waliyapata yamewasaidia kupata uelewa wa Sheria ya ya Chakula, dawa na vipodozi sura Na.219 na masuala mbalimbali yahusuyo chakula, dawa na vipodozi hivyo watakuwa mabalozi wazuri watakaowasaidia wananchi kupata uelewa juu ya masuala hayo.

“ Elimu niliyoipata imenisaidia na kupitia elimu hii kuhusu masuala ya chakula, dawa na vipodozi mimi kama mwandishi nitakuwa balozi mzuri ili kuwasaidia wananchi kujua madhara ya bidhaa zisizo salama kwa afya ya binadamu” alisema Shushu Joel kutoka Simiyu.

“Mafunzo haya yatatusaidia waandishi habari kujikita katika kuandika habari za kiuchunguzi zitakazowasaidia wananchi kujua madhara ya bidhaa zisizo salama kwa afya ya binadamu ” alisema Frankius Cleopas Mwandishi kutoka mkoani Mara.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/05/rc-mtaka-ashauri-tfda-kufungua-ofisi-za.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa