Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe.Gabriel Zakaria,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Bracius Chatanda na OCD wa Busega,leo wamewatembelea na kuwapa pole familia ambazo zilipoteza ndugu zao,kwenye ajali iliyotokea 11/1/2022 katika Kijiji cha Kalemela, Wilayani Busega na kusababisha vifo vya watu 15 hadi sasa.
Wakazi wa Kijiji cha Kalemela pamoja na maeneo ya jirani wamepoteza ndugu, jamaa na marafiki wapatao 9 na kufanya Mkoa wa Simiyu kupoteza jumla watu 9 kupitia ajali hiyo.Aidha Mhe.Kafulila amewapatia Salam za pole toka kwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na ubani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mwisho.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa