• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RAS Simiyu Awataka Waajiri Sekta Binafsi Kuwasilisha Madeni ya Michango ya Waajiriwa NSSF

Posted on: September 3rd, 2020

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga leo amefanya kikao na  Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF na baadhi ya waajiri wa sekta binafsi mkoani Simiyu kwa lengo la kujadili ulipaji wa madeni ya michango ya waajiriwa NSSF, ambapo katika kikao hicho imeazimiwa kuwa waajiri wote wa sekta binafsi wanaodaiwa wahakikishe wanalipa madeni hayo kwa wakati.

Akizungumza na waajiri wa sekta binafsi katika kikao hicho Bi Mmbaga amesema suala malipo ya michango ya mfuko wa hifadhi ya jamii ni suala la kisheria na lina manufaa kwa pande zote mbili (waajiri na waajiriwa), hivyo ni vema  NSSF iendelee  kutoa elimu ili kila upande ujue na utimize wajibu wake.

“Jambo hili lipo kisheria na lina faida kwa pande zote mbili mwajiri na mwajiriwa, kwa mwajiri kwamba hatasumbuliwa kwamba amekiuka sheria lakini mwajiriwa akiwa mwajiri  anayelipiwa michango yake ya pensheni  atatambua kuwa mwajiri wake anajali maslahi yake,”alisema Mmbaga.

Aidha, Mmbaga amesema azimio jingine la kikao hicho ni  Mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF Mkoa wa Simiyu kuhakikisha kuwa unatoa vitambulisho vya waajiriwa ambao waajiri wao wametimiza masharti ya kuanza kuwalipia michango ya mfuko wa hifadhi ya jamii mpaka kufikia Septemba 10, 2020 .

Wakati huo huo Mmbaga amesema Mkoa utaendelea kufanya vikao  na wadau angalau mara tatu  kwa mwaka kwa lengo la kuelimieshana na kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo namna sahihi ya utatuzi wa changamoto mbalimbali ili waweze wadau waweze kufanya kazi zao kwa tija na kuendana na dira ya mkoa yenye lengo la kuwa mkoa shindani kiuchumi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF, Bw. Nuru Mmbaga amesema  ni wajibu wa kila mwajiri katika sekta binafsi kulipa michango ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa kutoa asilimia 10 ya mshahara ghafi wa mwajiriwa nay eye mwajiri kulipia asilimia 10 pia kwa mujibu wa sheria.

Naye Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Mwanahamisi Kawega amesisitiza umuhimu wa waajiri kulipa madeni ya michango ya waajiriwa wao kwa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF ili waajiri wao waweze kupata haki na stahili zao mathalani mafao ya uzazi.

Kwa upande wao waajiri wa sekta binafsi walioshiriki katika kikao hicho wameshukuru uongozi wa Mkoa kuitisha kikao hicho ambapo wamekiri kuwa wako tayari kulipa madeni yote halali ya michango ya waajiriwa wao huku wakisisitiza elimu iendelee kutolewa kwa waajiri na waajiriwa ili wawe na uelewa wa pamoja kuhusu haki na wajibu wao katika masuala ya hifadhi ya jamii.

“Tunashukuru kwa kikao kizuri ambacho umekuwa na mjadala mzuri, sisi tuko tayari kulima madeni hayoa lakini kinachotakiwa ni NSSF kutusaidia kutoa namba za utambulisho maana watumishi wetu wengi  walikataa fedha zao kukatwa kutokana na kutokuwa na namba, tunaombba namba zitolewe kwa wakati,” alisema Bi.Tina Chenge Mkurugenzi wa Madina Bakery Company.

“Tunaomba elimu kwetu na kwa watu wetu iendelee kutolewa maana tunafanya kazi tofauti na tunaajiri watu kwa namna tofauti mfano katika viwanda kuna waajiriwa tunakuwa nao kwa miezi miwili au mitatu, nashauri tukae chini tuangale madeni yote halali tulipe na NSSF itoe kadi za utambulisho kwa waajiriwa wetu ambao tuanze kuwalipia michango yao mara moja,” alisema Gungu Silanga Mkurugenzi kampuni ya Nsagali.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/09/ras-simiyu-awataka-waajiri-sekta.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa