• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Profesa Ndalichako:Wizara ya Elimu haina Urasimu kusajili Shule ikiwa Vigezo Vimezingatiwa

Posted on: December 28th, 2017

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Wizara yake haina urasimu wowote katika usajili wa shule ikiwa vigezo vyote vinavyotakiwa vimezingatiwa katika uanzishwaji wa shule hizo.

Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo jana wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi katika Shule Shikizi/tarajali ya Njalu iliyopo Habiya Wilayani Itilima na alipotembelea shule ya Sekondari ya Chegeni inayotendelea kujengwa Kijiji cha Bulima Wilayani Busega  zote zikiwa zinajengwa kwa nguvu ya wananchi.

“Lengo la Serikali ni kuwa na shule nyingi lakini ni lazima vigezo na masharti yaliyowekwa na Wizara yazingatiwe; Kuna watu ambao siyo waaminifu, zamani ilikuwa hata mtu akiwa na madarasa matatu akiomba usajili anaruhusiwa na shule inasajiliwa lakini wakisharuhusiwa wanabweteka na matokeo yake wanaleta shida kwa watoto wetu” alisema Profesa Ndalichako

Ameongeza kuwa Wadhibiti ubora wapewe nafasi ya kushiriki katika vikao vya Mabaraza ya madiwani ili waweze kutoa elimu na mwongozo kwa madiwani juu ya mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa wanapotaka kuanzisha shule katika maeneo yao na wataalam wa elimu wasaidie katika kutoa elimu juu ya miongozo na vigezo vyote.

Aidha, amewapongeza wananchi wa Habiya Itilima na Bulima Busega kwa kuchangia nguvu na michango yao katika  kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli kwenye ujenzi wa shule hizo na akawataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanakwenda wasiwape majukumu mengine.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mbunge wa Itilima Mhe.Njalu Silanga na Mbunge wa Busega, Mhe.Dkt.Raphael Chegeni wamesema wananchi katika maeneo zilizopo shule hizo wako tayari kuunga mkono Juhudi za Serikali katika ujenzi wa shule,  hivyo wakaomba watakapokamilisha ujenzi wa miundombinu kulingana na miongozo waliyopewa wasajiliwe shule hizo ili kutoa nafasi kwa watoto kupata mahali pa kujifunzia.

“Mhe.Waziri tunakubali kufuata maelekezo yako na tunaomba tutakapo kamilisha mahitaji tunaomba shule hii iweze kusajiliwa na katika Jimbo langu kuna shule 22 za aina hii ambazo zimejengwa kwa nguvu za wananchi” alisema Njalu Silanga Mbunge wa Itilima.

Pamoja kutoa maelekezo na mwongozo kwa wananchi Mhe. Waziri wa Elimu ameahidi kuchangia ujenzi wa shule hizo kwa kutoa saruji mifuko 100 kwa Shule ya Njalu(Itilima) na Mifuko 150 kwa Shule ya Chegeni (Busega) na kuwataka Wakurugenzi wa Halmashauri hizo kuhakikisha kuwa wanatafuta vifaa vingine ili kukamilisha miundombinu inayotakiwa kwa kushirikiana na wananchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali ya Mkoa na Wilaya ya Itilima itachangia  saruji mifuko 100 kwa shule ya Msingi (shikizi) Njalu (Itilima) na Serikali ya Mkoa na Wilaya ya Busega itachangia mifuko 50 kwa Shule ya Sekondari Chegeni(Busega) .

Shule ya Msingi Njalu (Shikizi) hadi sasa ina vyumba vya madarasa vitano, ofisi moja ya walimu  na ina upungufu wa chumba kimoja cha darasa, ofisi ya walimu 01 pamoja na matundu ya vyoo matano (05) na mpaka sasa Mbunge wa Jimbo la Itilima ametoa zaidi ya milioni 26 kuwaunga mkono wananchi.

Kwa upande wa   Shule ya Sekondari ya Chegeni inayoendelea kujengwa mpaka sasa  ina vyumba viwili vya madarasa, ofisi moja ya walimu, ina upungufu wa vyumba viwili vya madarasa, vyumba vitatu vya maabara, matundu 10 ya vyoo, maktaba, jengo la utawala na nyumba mbili za walimu ambapo hadi sasa Mbunge wa Busega Dkt.Raphael Chegeni ameshangia jumla ya shilingi  milioni 10 katika kuwaunga mkono wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Busega Mhe.Dkt.Raphael Chegeni akizungumza na wananchi wa Bulima wakati Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa.Joyce Ndalichako alipotembelea shule ya Sekondari inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambayo imepewa jina la Mbunge huyo (Chegeni Sekondari) jana.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa.Joyce Ndalichako akiweka Jiwe la Msingi Vyumba vya Madarasa  vya Shule ya Msingi iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na kupewa jina la Mbunge Njalu(Shule ya msingi Njalu) iliyopo Habiya wilayani Itilima wakati wa ziara yake jana.


Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe.Njalu Silanga akizungumza katika uwekaji wa Jiwe la Msingi la Vyumba vya Madarasa Shule ya Msingi Njalu (Shule shikizi) iliyoko Habiya wilaya ya Itilima wakati wa Ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa.Joyce Ndalichako wilayani humo jana.

Diwani ya Kata ya Nyashimo na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akizungumza na wananchi wa Bulima wakati Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa.Joyce Ndalichako alipotembelea shule ya Sekondari inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambayo imepewa jina la Mbunge wa Busega Dkt.Raphael Chegeni (Chegeni Sekondari) jana.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Bulima Kata ya Nyashimo wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa.Joyce Ndalichako wakati alipopita kuona ujenzi wa shule ya sekondari Chegeni ambayo inajengwa kwa nguvu ya wananchi hao wilayani Busega.

Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa.Joyce Ndalichako, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka, Diwani ya Kata ya Nyashimo na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mickness Mahela, Mkurugenzi Busega na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu wakifurahia jambo wakati wa Ziara ya Waziri wa Elimu wilayani Busega.

Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa.Joyce Ndalichako wakiteta jambo wakati wa ziara ya Mhe.Waziri wa Elimu wilayani Itilima jana.

Kutoka kushoto Mbunge wa Jimbo la Busega Mhe.Dkt.Raphael Chegeni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa.Joyce Ndalichako, Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mickness Mahela, Mkurugenzi wa Busega Anderson Njiginya wakifurahia jambo  wakati wa Ziara ya Waziri wa Elimu wilayani Busega.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Habiya mara baada ya kukwa nguvu ya wananchi  katika Shule ya msingi Njalu(Shule shikizi) wakati wa ziara yake wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa