• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

NSSF Yaridhia kutoa Shilingi Bilioni 1.5 Upanuzi Kiwanda cha Chaki Maswa

Posted on: May 3rd, 2017

Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF imeridhia kutoa mkopo  wa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki kilichopo wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Meneja wa Mipango na Uwekezaji wa NSSF  Bibi. Radhia Tambwe katika mahojiano maalum na waandishi wa Habari mara baada ya kikao cha wadau wa uwekezaji Mkoani Simiyu kilichofanyika Kata ya Lamadi wilayani Busega ambacho kimewahusisha wadau mbalimbali wa uwekezaji mkoani humo.

Bibi.Radhia amesema Bodi imefanya uamuzi huo baada ya kupitia maombi ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na kuona kuwa mradi wa kiwanda cha chaki una tija kwa kuwa umewashirikisha vijana hivyo kiwanda kitakapopanuliwa kitaongeza wigo wa ajira kwa vijana, pato la wilaya na kuokoa fedha za kigeni zinazotumika kuagiza chaki nje ya nchi.

Aidha, amepongeza utekelezaji wa Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja” mkoani Simiyu katika Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda ambapo amesema kupitia viwanda vitakavyoanzishwa katika kila wilaya chini ya Kauli Mbiu hii mkoa utatengeneza ajira kwa wananchi wa ndani na nje ya mkoa.

Bi. Radhia pia ametoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono miradi ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani Simiyu kwa kuwa ni miradi yenye tija kwa kuzingatia kuwa  malighafi zinazotumika zinapatikana hapa nchini na soko lake kubwa liko hapa nchini.

“Watanzania tubadilike tusikubali kila mara kugeuzwa supermarket, tuzalishe bidhaa zetu na kutumia bidhaa zetu wenyewe tujivunie tulivyonavyo ili tuweze kuendeleza nchi yetu na hatimaye Tanzania na sisi tuwe nchi yenye uchumi wa kati” alisema.

Naye  Mkurugenzi wa Benki ya Azania Ndg.Charles Jackson Itembe amesema benki hiyo iko tayari na inaunga mkono uwekezaji katika sekta ya viwanda unaofanywa na Halmashauri za Mkoa wa Simiyu chini ya Kauli mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja” kwa kutoa uwezeshaji kifedha katika miradi iliyoaanishwa na Halmashauri husika kupitia mikopo.

Kwa upande wake Mtaalam Mbobezi wa Viwanda, Ndg. Ndaki Munyeti amesema Mkoa wa Simiyu umejipanga na kuwashirikisha Wataalam mbalimbali katika kuchagua teknolojia itakayotumika katika viwanda vilivyopo na vitakavyoanzishwa ambayo ndiyo hatua muhimu katika ujenzi wa viwanda inayoweza kusaidia kupata bidhaa bora na kufanya viwanda vikawa endelevu.

Awali akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha wadau wa uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu Mkuu wa Mkoa huo, Anthony Mtaka amesema pamoja na NSSF na Benki ya Azania kukubali kuunga mkono juhudi za Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani Simiyu amesema Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wameahidi kutoa fedha za upembuzi yakinifu kwa mradi utakaotekelezwa katika kila wilaya.(Wilaya Moja Bidhaa Moja)

Mtaka amewataka viongozi kila mmoja awajibike ipasavyo katika eneo lake kwa kuwa wale walioteuliwa waliaminiwa na Mhe.Rais na waliochaguliwa waliaminiwa na wananchi hivyo watimize wajibu wao kuhakikisha viwanda vinasimama na kero za wananchi zinatatuliwa.

“Viongozi wenzangu wa kuteuliwa tunapaswa kuwajibika, Mhe.Rais aliacha watu wengi akatuamini akatuteua sisi, Waheshimiwa madiwani wananchi waliwaamini kuwachagua, ni lazima tuioneshe dunia kuwa inawezekana; natamani mwaka 2020 tutengeneze kura siyo mikutano ya hadhara, kila atakapo pita Mhe.Rais kuwe na kitu ambacho wananchi wanajivunia kupitia kazi zetu sisi” alisema.

Kikao cha wadau wa uwekezaji kiliwahusha wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Watalaam wa Sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya,Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi wa Halmashauri,Wajumbe wa Kamati za Fedha za Halmashauri, Maafisa Mipango, Wachumi, Wataalam kutoka Benki ya Azania, NSSF na Watalaam wa Viwanda na Masoko.

Katika kikao hicho maandiko ya miradi ya uanzishwaji viwanda kutoka katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu yaliwasilishwa kwa wadau hao ambayo ni upanuzi wa kiwanda cha chaki na kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya karatasi (Maswa), upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, kiwanda cha kutengeneza sabuni za maji, mche na unga Itilima, kiwanda cha kutengeneza tomato sauce na chili sauce (Busega) kiwanda cha kusaga nafaka  na kufungasha unga pamoja na unga lishe (Bariadi Mjini) na kiwanda cha kutengeneza bidhaa za Ngozi (Halmashauri ya Wilaya Bariadi) lengo likiwa ni wadau wa Taasisi za fedha na watalaam kwa pamoja kupitia maandiko hayo kujiandaa na utekelezaji.

Upanuzi wa Kiwanda cha Chaki ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Uongozi wa Wilaya ya Maswa baada ya kutembelea kiwanda hicho wakati wa ziara yake mwezi Januari wilayani Maswa Mkoani Simiyu, ambapo aliagiza uongozi huo kukopa fedha kwa ajili kupanua kiwanda hicho ili kuongeza uzalishaji.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa