• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

NEC Kuanza Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Julai 31, Mkoani Simiyu

Posted on: July 21st, 2019

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Simiyu kuanzia  Julai 31, 2019 hadi Agosti 06, 2019 ambapo zoezi hilo kitaifa lilizinduliwa rasmi Julai 18, 2019.

Akifungua mkutano wa wadau wa Uchaguzi mkoani Simiyu, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage amesema Tume imekamilisha maandalizi ya uboreshaji daftari ambayo ni pamoja na kuhakiki vituo vya kujiandikisha, uandikishaji wa majaribio, maandalizi ya vifaa vya uboreshaji daftari, mkakati wa elimu kwa mpiga kura na uzinduzi wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Amesema uboreshaji huu hautawahusisha wapiga kura wote walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2015 bali utawahusu wapiga kura wapya ambao wametimiza miaka 18, wale ambao watatimmiza.umri wa miaka 18 siku ya uchaguzi Mkuu mwaka 2020, ambao wamehama katika maeneo ya awali ya uchaguzi na wale ambao kadi zao zimeharibika

Katika hatua nyingine Jaji Kaijage ametoa rai kwa wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kuboresha taarifa zao, huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa, kuzingatia sheria za uchaguzi na kanuni zake katika zoezi hili la uboreshaji na maelekezo kwa Vyama vya Siasa kuhusu uboreshaji.

Kwa upande wake Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Frank Mhando amesema Tume imefanya uhakiki wa vituo vya uandikishaji ambavyo vimeongezeka kutoka 36,549 mwaka 2015 hadi 37,407 mwaka 2018 (Tanzania Bara), upande wa Tanzania Zanzibar vimeongezeka kutoka 380 mwaka 2015 hadi 407 mwaka 2018; huku akifafanua kuwa katika uandishaji huu kila Kijiji au Mtaa utakuwa na angalau Kituo kimoja cha kujiandikisha.

Naye Mratibu wa Zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Simiyu, Bw. Maganga Simon amesema mkoa umejiandaa vizuri ili kufanikisha zoezi ambapo wananchi wenye sifa zaidi ya 700,000 wanatarajia kuandikishwa katika daftari hilo huku akiwasisitiza viongozi wote mkoani hapo kuwahamasisha wananchi wenye sifa kujitokeza kujiandikisha.

“Mkoa wetu ni mwenyeji wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka2019, tutatumia fursa hiyo kuhamasisha, kutakuwa na bango kubwa litakaloonesha kuwa kuanza Julai 31 hadi Agosti 6 2019 mkoa wetu utashiriki kikamilifu kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na Simiyu tumejipanga kufanikisha zoezi hili ambalo linasimamiwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi” alisema

Akizungumza kwa niaba ya watu wenye ulemavu,  Katibu wa Chama cha Viziwi (CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Alex Benson amewaomba viongozi wa vyama vya siasa kuwapa fursa watu wenye ulemavu kuwania nafasi mbalimbali, huku akisisitiza wasimamizi kupewa mafunzo ya lugha ya  alama ili kurahisisha mawasiliano  na watu wenye ulemavu pindi wanapoenda kujiandikisha na kupiga kura.

Naye Dora Stephano kutoka katika ASASI za kiraia amesema Tume ione uwezekano wa kuongeza ushirikishwaji wa asasi za kiraia nyingi zaidi, ili kuongeza wigo wa kutoa elimu kwa wapiga kura juu ya masuala mbalimbali ya uandikishaji na uchaguzi.

Mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Simiyu, umewahusisha Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa, Viongozi wa Vyama vya siasa Viongozi wa dini, wawakilishi wa watu wenye ulemavu, wawakilishi wa vijana, wawakilishi wa wanawake, wawakilishi wa asasi za kiraia, watendaji wa Tume na waandishi wa habari.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/07/nec-kuanza-uboreshaji-wa-daftari-la.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa