Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa wito kwa Halamshauri zote nchini kubuni miradi ya kimkakati ya itakayoziongezea mapato badala ya kuendelea kutegemea ushuru na tozo mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Dkt. Kijaji amayasema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza chaki cha wilaya ya Maswa wakati wa ziara yake ya kujionea utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Vwanda Mkoani Simiyu akiwa na viongozi wa Halmashauri na Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa.
Amesema Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Halmashauri zote zinabuni miradi ya kimkakati ambayo itaziongezea mapato na akatoa wito kwa Halmashauri zote nchini kujifunza kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambayo imetengewa shilingi bilioni 8.2 na Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi miwili ya upanuzi wa Kiwanda cha Chaki na kujenga kiwanda cha vifungashio.
“Niwapongeze Simiyu mnafanya kazi nzuri, tunataka kuondoka kwenye ule ukawaida wa Halmashauri zetu kulalamika kuwa Serikali Kuu imechukua vyanzo vya mapato, Serikali Kuu haijachukua kinachohitajika ni ubunifu wa miradi kama Halmashauri ya Maswa ilivyofanya, nitoe wito kwa Halmashaui zote kubuni miradi, Serikali ipo tayari fedha zipo kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya kuongeza mapato ya Halmashauri” alisema
Mbunge wa Maswa Mashariki na Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo ameiomba Serikali kutoa fedha hizo shilingi Bilioni 8.2 zilizotengwa kwa wakati ili Miradi iliyokusudiwa ya upanuzi wa kiwanda cha chaki na ujenzi wa kiwanda cha vifungashio iweze kutekelezwa kwa wakati.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema katika kukiongezea kiwanda cha chaki uwezo wa uzalishaji, Halmashauri ya Maswa imenunua eneo ambapo malighafi ya kutengenezea chaki inapatikana, katika Mkoa wa Singida.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dkt. Fredrick Sagamiko amesema Halmashauri hiyo imedhamiria kufikisha zaidi ya asilimia 75 ya mapato ya ndani yatakayotokana na viwanda vilivyopo na vinavyoendelea kujengwa wilayani humo.
Awali Dkt. Ashatu alitembelea eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika viwanda la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mahali ambapo patajengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza chak(upanuzi wa hiki kilichopo) na kujenga kiwanda cha vifungashio
MWISHO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa mkoani Simiyu ambapo aliongozana na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa sera ya viwanda mkoani humo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kulia)akiangalia viatu vya ngozi vinavyotengenezwa katika kiwanda cha Senani wilayani Maswa mkoani Simiyu baada ya kutembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa akiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa sera ya viwanda
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji chupa ya maziwa ya Meatu wakati wa ziara yake mkoani humo akiwa na viongozi wa Halmashauri ya Kondoa na viongozi wa CCM wilaya ya Kondoa mkoani humo kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda mkoani humo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akisaini ubao kwa kutumia chaki za Maswa katika kiwanda cha chaki Maswa mkoani Simiyu, baada ya kutembelea kiwanda hicho akiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa sera ya viwanda mkoani humo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akionesha risiti ya EFD baada ya kununua chaki za Maswa mkoani Simiyu, baada ya kutembelea kiwanda cha chaki akiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza mkoa wa Simiyuunavyotekeleza sera ya viwanda.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Kiwanda cha Maswa(waliochuchumaa), viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu kutembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa akiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza mkoa wa Simiyu unavyotekeleza sera ya viwanda.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akisaini ubao kwa kutumia chaki za Maswa katika kiwanda cha chaki Maswa mkoani Simiyu, baada ya kutembelea kiwanda hicho akiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza mkoa wa Simiyu unavyotekeleza sera ya viwanda.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa chupa ya maziwa ya Meatu wakati ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wa Halmashauri hiyo na viongozi wa CCM wilaya ya Kondoa mkoani Simiyu kwa ajili ya kujifunza mkoa wa Simiyu unavyotekeleza Sera ya Tanzania ya Viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea eneo la uwekezaji wa viwanda wilayani Maswa ambapo aliongozana na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa sera ya viwanda mkoani humo.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa