• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Waziri Silinde Aridhishwa Ujenzi wa Bwalo, Madarasa Sekondari ya Anthony Mtaka Busega

Posted on: March 6th, 2021

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David Silinde ameridhishwa na namna mradi wa ujenzi wa bwalo, vyumba viwili vya madarasa, maabara na matundu ya vyoo ulivyotekelezwa kwa viwango katika Shule ya Sekondari Anthony Mtaka iliyopo kata ya Lamadi wilayani Busega Mkoani Simiyu.

Silinde ameyasema hayo leo Machi 06, 2021 shuleni hapo alipotembelea mradi huo wakati wa ziara akikamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo mabweni, mambwalo, madarasa na matundu ya vyoo.

“Nimeisikiliza hii ripoti iliyosomwa na Mkuu wetu wa shule, nimekagua madarasa, maabara nimekagua na bwalo la chakula kwa kweli mmejenga kwa viwango vinavyoridhisha kikubwa zaidi mmekuwa na usimamizi mzuri wa fedha za serikali, kwa  kazi iliyofanyika hapa hiyo milioni 42 iliyosomwa hapa kama bakaa mnaweza mkaitumia kukamilisha madarasa mengine yaliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi,” alisema.

Ameongeza kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI imedhamiria kudhibiti mapato na matumizi ya fedha za Serikali huku akiwataka watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa wazalendo na waadilifu katika usimamizi wa fedha za serikali na kuhakikisha wanapopewa fedha kwa aajili ya utekeelzaji wa miradi watekeleze kwa mujibu wa maelekezo wanayopewa.

Aidha, Silinde amesema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuboresha miundombinu ya elimu kwa ajili ya kuboresha mazingira ya utoaji elimu kwa watoto wa Kitanzania na ndiyo maana sasa hivi imejikita katika ujenzi wa mabweni bora, madarasa bora, mabwalo bora, maabara za kisasa na matundu ya vyoo bora na kuahidi kuwaondoa kwenye nafasi zao wale wote wenye nia ya kuikwamisha serikali.

Naye Mbunge wa Jimbo la Busega, Mhe. Simon Songe ameishukuru Serikali kwa fedha ilizotoa kwa jili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu wilayani Busega na kuahidi kuendelea kuzisimamia fedha hizo ili ziweze kutimiza azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Songe ameongeza kuwa wilaya ya Busega ina mahitaji ya shule 44 za sekondari zilizopo zikiwa 20 na ambazo zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni zikiwa nne, hivyo ameomba Serikali itakapoombwa fehda kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za wananchi katika ujenzi wa shule hizo itoe kipaumbele kwa wilaya hiyo ili kufikia lengo la kuwa na shule 44 za sekondari.

Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya sekondari Anthony Mtaka wanaishukuru serikali kwa kuwajengea madarsa, bwalo na maabara jambo ambalo wamekiri kuwa litachangia katika kuboresha mazingira yao ya kujifunzia.

“Tunaishukuru serikali kutujengea maabara ambayo itatusaidia sana kufanya mazoezi ya vitendo hususani kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi lakini na madarasa tuliyongewa tunashukuru pia maana yamepunguza msongamano darasani,” alisema George Daud kiranja Mkuu Anthony Mtaka sekondari.

“Pamoja na kutujenge madarasa maabara na vyoo mimi ninaishukuru serikali kwa kutujengea bwalo ambalo tutalitumia kwa matumizi mbalimbali zaidi ya kulia chakula, tutalitumia kufanyia mikutano na midahalo; hili litakuwa mkombozi maana tulikuwa tunafanyia vikao vyetu na midahalo chini ya miti,” alisema Sarah Mathias mwanafunzi shule ya sekondari Anthony Mtaka.

Awali akiwasilisha taarifa Mkuu wa Shule ya Sekondari Anthony Mtaka, Mwl. Joseph Kazimoto amesema fedha zilizopokelewa ni shilingi 196, 600,000/= kwa lengo la ujenzi wa bwalo, vyumba viwili ya madarasa, maabara na matundu sita ya vyoo na mara baada ya kukamilisha kazi hizo fedha iliyobaki ni jumla ya shilingi 42,894,100/= .

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2021/03/naibu-waziri-silinde-aridhishwa-ujenzi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa