• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Waziri Mgumba: Meatu Mmechaguliwa Kuzalisha Mbegu za Pamba Zigatieni Kanuni za Kilimo Bora tupate Mbegu Bora

Posted on: March 8th, 2019

Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba amewataka wakulima wa pamba kata ya Mwabusalu wilayani meatu Mkoani Simiyu iliyochaguliwa kuzalisha mbegu za pamba kuzingatia kanuni za kilimo bora lengo likiwa kupata mbegu bora zitakazotumika katika maeneo yanayolima zao hilo hapa nchini.

Ameyasema hayo akiwa kwenye ziara ya kikazi wilayani hapo yenye lengo la kukagua shughuli za kilimo, kusikiliza kero za wakulima katika kujiletea maendeleo wakati akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya mwabusalu iliyopo wilayani hapo.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Kilimo Mgumba, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani amesema kuwa bado wanaendelea kutoa elimu kwa wakulima waliopewa dhamana ya kuzalisha mbegu za pamba kutochanganya mazao huku akiongeza kuwa mbegu hiyo itazalishwa ya kutosha.

“Mbegu inazalishwa hapa Mwabusalu na baadaye inapelekwa maeneo mengine yanayolima pamba nchini, isingependeza kukawa na maotea kwenye eneo ambalo limepewa dhamana ya kuzalisha mbegu, tunaendelea kuwaelimisha wakulima na kuhakikisha kuwa maotea yasiwe sehemu ya pamba itakayonunuliwa kwa ajili ya mbegu” alisema Dkt. Chilongani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mkuu wa Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Meatu na Kamati yote ya Ulinzi na Usalama isimamie operesheni ya kuondoa maotea kwenye mashamba ya pamba iliyokuwa imesitishwa ili kulinda ubora wa mbegu na mfumo wa kuzalisha mbegu za pamba.

“Tulikuwa tunaendesha operesheni ya kuhakikisha mashamba yote ya kuzalisha mbegu hapa Mwabusalu yanazingatia taratibu za kuzalisha mbegu, ilisitishwa kutokana na vitisho vya wana Mwabusalu kutaka kuwapiga waliokuwa wakipita kwenye mashamba kuondoa maotea, Mhe. DC kuanzia kesho Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya isimamie zoezi hili ili tusipoteze mfumo wa kuzalisha mbegu bora” alisema Mtunga”

Baadhi ya wakulima wa pamba katika Kata ya Mwabusalu wameiomba Serikali kuendelea kuwapata pembejeo kwa wakati na kutoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuwaongoza katika kuzingatia kanuni za kilimo bora badala ya kuwapotosha  ili waweze kulima kwa tija na kutoka kwenye umaskini.

“Ninaomba Serikali iendelee kutoa madawa na mbolea kwa wakati ili tuweze kuzalisha kwa tija maana mwaka huu tumeongeza uzalishaji na tunatarajia mavuno mengi kwa kuwa pamba haijashambuliwa sana na wadudu kama mwaka jana” alisema Charles Thomas mkulima Mwabusalu

“Baadhi ya viongozi wa kisiasa waache kuhubiri habari mbaya kwenye kilimo cha pamba  maana hawahubiri suala la kufuata sheria, mfano wanapotuambia tuchanganye pamba na mazao mengine wakati wataalam wanasema haitakiwi je wanatusaidia kutoka kwenye umaskini au wanataka tuendelee kuwa maskini” alisema Bupolo Mahangi

Akijibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa kwenye mkutano huo Naibu Waziri Mgumba amewataka baadhi ya wanasiasa kuwa sehemu ya kutoa elimu na kuwaongoza wakulima hao kuzingatia kanuni za kilimo bora ili waweze kulima kwa tija, kuzalisha mbegu bora na kuongeza mavuno.

Naibu Mgumba jana amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Simiyu kwa kutembelea mradi wa kilimo cha umwagiliaji, kutembelea mashamba ya pamba na kuzungumza na wananchi wilayani Maswa, akiwa wilaya Meatu alitembelea shamba la kuzalisha mbegu za pamba na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo la Mwabusalu lililopo wilayani hapo.

MWISHO

 KUPTA PICHA ZAIDI KAMILI FUNGUA KIUNGNISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/03/naibu-waziri-mgumba-meatu-mmechaguliwa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa