Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula ameshauri Wizara ya Viwand, Biashara na Uwekezaji kuona namna ya kuwa na Kliniki za Biashara ngazi ya kanda ili kuwasaidia wafanyabiashara hususani wale wanaoanza, wajasiriamali wadogo na wasiojua taratibu za uendeshaji wa biashara zao kujua na kuwa wafanyabiashara wazuri.
Mhe.Mabula ameyasema hayo mara baada ya kutembelea banda la Maonesho la Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TanTrade) katika Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yanayoendelea katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Amesema amepongeza Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji kubuni Kliniki ya biashara ambayo inachangia kuwandaa wafanyabiashara kufahamu wafanye nini kabla na baada ya kuanzisha biashara na kufanya biashara zao kwa kuzingata sheria, kanuni na taratibu za nchi hii
“Ili mtu awe huru kufanya biashara yake ni lazima zingatie sheria kanuni na taratibu za nchi hii, mtu anapokuja kwenye kliniki hii anaambiwa kabla ya kuanza anatakiwa apitie hatua zipi na aweke mazingira yapi, ili atambulike na TRA anapaswa afanye nini na mambo mengine mengi na wakizingatia wanachoambiwa hapa hawahitaji kukimbizana na mgambo wa polisi”
“Ninashauri Wizara ya Viwanda ione namna ya kuwa na kliniki za biashara kikanda ili wafanyabiashara wanaoanza, wajasiriamali wadogo na wale wasiojua taratibu waweze kujua taratibu na wawe wafanyabiashara wazuri” alisema Mhe. Mabula.
Afisa Biashara Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara hapa nchini (TanTrade) Bi. Magdalena Shirima amesema hadi kufikia Oktoba 26, 2018 wajasiriamali zaidi ya 60 walioshiriki katika Maonesho ya SIDO Kitaifa wamehudhuria Kliniki hiyo kupata huduma.
Baadhi ya Wajasiriamali waliopata nafasi ya kushiriki na kupata huduma za ushauri wa kibiashara kupitia Kliniki hiyo wamesema imewasaidia kubadili mitazamo dhidi ya biashara zao na kufahamu mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uanzishaji wa biashara, namna ya kutangaza biashara zao na umuhimu wa kusajili biashara zao ili ziweze kutambulika kisheria.
Maonesho haya ya Viwanda Vidogo (SIDO) ni ya kwanza Kitaifa yakiwa na Kauli Mbiu “Pamoja Tujenge Viwanda Kufikia Uchumi wa Kati” ambayo yalianza Oktoba 23, 2018 yatahitimishwa Oktoba 28, 2018.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/10/naibu-waziri-mabula-ashauri-wizara-ya.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa