• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Spika Afungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli Simiyu

Posted on: August 6th, 2017

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amefungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli na Ngoma za Asili Mjini Bariadi(Simiyu Jambo Festival) ambayo yamehudhuriwa na Maelfu ya Wananchi wa Mkoa wa Simiyu.

Mashindano hayo ya mbio za baiskeli yamehusisha kilometa 200 wanaume, kilomita 80 wanawake ambapo pia  walemavu waliweza kushindania katika umbali wa kilomita tano.

Akizungumza baada ya kufungua mashindano hayo Dkt.Tulia pamoja na kuupongeza Mkoa wa Simiyu kuandaa mashindano hayo amesema, ipo michezo nchini haijapewa kipaumbele lakini ikitumiwa vizuri inaweza kutoa ajira ukiwemo mchezo wa mbio za baiskeli; ambapo ametoa wito kwa viongozi wa mikoa mingine pia kuwekeza katika michezo mbalimbali ili kuwasaidia wananchi kupata kipato.

“Lililofanyika Simiyu ni jambo jema sasa hivi watu watakuwa wanajua kuwa wakijifua vizuri kwenye baiskeli na ngoma za jadi wanakuja kushiriki mashindano ya Baiskeli na  ngoma Simiyu, nitoe wito kwa viongozi wengine kufikiria mambo mengine yanayoweza kuwasaidia wananchi katika maeneo yao kupata ajira na kujipatia kipato” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema mkakati wa mkoa huo ni kurasimisha tamaduni zote na kuhusianisha na shughuli za Utalii ndani ya mkoa huo.

“Position(Nafasi) ya Mkoa wa Simiyu kwenye nchi ni kukuza tamaduni na sanaa zetu kama moja ya eneo litakalotuunganisha na sekta ya Utalii, tumezungukwa na mapori ya akiba na mbuga za wanyama, tungehitaji watalii wanapokuja kwenye maeneo hayo wapate ladha ya tofauti kiwemo utamaduni wa Mtanzania”

Mtaka ameongeza kuwa wasanii wote watatambuliwa na baadae kujengewa uwezo  kupitia watalaam wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(Kitivo cha sanaa),Chuo cha Sanaa Bagamoyo na vyuo vya michezo ili waweze kufanya kazi zao kibiashara na kuimarisha uchumi wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Mhe.Salum Khamis ambaye ndio Mdhamini wa mashindano ya Baiskeli na ngoma za Asili (Simiyu Jambo Festival) amesema ataendelea kudhamini mashindano kama hayo Mkoani Simiyu ili kuwawezesha wananchi kuinua kipato kupitia vipaji vyao.

 Naye mshindi wa kwanza mbio za kilometa 80 (wanawake) Raulensia Luzuba kutoka Mwanza ameomba mashirika na makampuni mbalimbali kuwadhamini ili waweze  kujengewa uwezo na kuandaliwa kushiriki katika mashindano ya Kimataifa.

Masunga Duba mshindi wa mbio za kilometa 200(wanaume)kutoka Simiyu amesema pamoja na wafadhili kudhamini mashindano wawasaidie  pia wachezaji kupata baiskeli za kisasa zitakazowasaidia kwenda kwa kasi inayotakiwa.

Mashindano ya baiskeli Mkoani Simiyu yameshirikisha wachezaji kutoka mikoa ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga,Arusha na Mbeya, ambapo ushindi kwa upande wa wanaume umechukuliwa na Hamisi Hussein(Arusha) ambaye amejishindia pikipiki, wa pili ni Masunga Duba(Simiyu) kitita cha shilingi 1,000,000/= wa tatu Richard Laizer(Arusha) .shilingi 500,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 15.

Kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza  Raulensia Luzuba kutoka Mwanza amejipatia shilingi 500,000/=, mshindi wa pili Tatu Malulu(Mwanza) shilingi 400,000/= na wa tatu ni Vumilia Mwinamila(Simiyu) shilingi 300,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 10.

Walemavu mshindi wa kwanza Emmanuel Mtemi amejipatia shilingi 200,000/= wa pili Masunga Sendama shilingi 150,000/= na wa tatu Saguda Sospeter shilingi 100,000/=wote kutoka mkoa wa Simiyu na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne na wa tano.

Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye baiskeli wa pili kulia) akiwa na viongozi wa Mkoa na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu na Viti Maalum kutoka nje ya Mkoa kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi.

Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (wa pili kushoto) akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi (kulia) ni Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products ambayo ni mdhamini, Mhe.Salum Khamis akimpongeza Mshindi huyo


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa