Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 umeanza mbio zake Mei 22, 2019 Mkoani Simiyu ambapo unatarajia kupitia miradi 34 kutoka katika sekta binafsi, maji, elimu, afya, viwanda, kilimo, barabara, maendeleo ya jamii na hifadhi ya mazingira ambayo ina thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.8.
Akizungumza mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mwanza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema katika thamani hiyo ya miradi ambayo ni shilingi 8, 878,598,412.25 shilingi 904,170,725.00 ni nguvu za wananchi, Halmashauri shilingi 428, 403,532.63, Serikali Kuu ni shilingi 5, 992,582,072.37, wahisani shilingi 1,256,475,082.25 na sekta Binafsi shilingi 296,967,000.00
Akizungumzia Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 “MAJI NA HAKI YA KILA MTU TUTUNZE VYANZO VYAKE NA TUKUMBUKE KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA” Mtaka amesema, wastani wa upatikanaji maji Simiyu ni asilimia 50.4 ambao unahudumia wakazi 817, 968 na kubainisha kuwa Serikali inaendelea kuhamasiha wananchi kulinda vyanzo vya maji ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo.
Aidha, amesema Mkoa wa Simiyu umejipanga na unaendelea kuandaa mazingira mazuri ya amani na utulivu, yatakayowezesha wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali amewataka viongozi wa mkoa wa Simiyu na wilaya zote mkoani humo kuhakikisha taarifa zote za miradi ya maendeleobitakayopitiwa na Mwenge wa uhuru ziwepo eneo la mradi na wataalam wote wanaohusika na miradi hiyo wawepo.
Baada ya kupokelewa Mkoani Simiyu Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake wilayani Maswa ambapo umepitia mradi wa urasimishaji wa makazi Malampaka, ukaguzi wa ujenzi wa barabara za lami Mjini Maswa, mradi wa maji Nyashimba, Kiwanda cha viazi lishe Njiapanda, vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja Kijiji cha Mwadila.
Aidha, Mwenge wa Uhuru ulitembelea na kuona shughuli za wajasiriamali na kutoa hundi za wajasiriamali, kuzindua klabu za kutokomeza rushwa na dawa za kulevya, kuzindua kampeni ya tokomeza malaria na kukagua shughuli za utoaji elimu ya kuhimiza upimaji wa VVU/UKIMWI.
Mwenge wa Uhuru takimbiza kwa mua wa siku sita mkoani Simiyu Mei 22 mpaka Mei 27, 2019 na Mei 28, 2019 utakabidhiwa mkoani Mara.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU NA MBIO ZAKE WILAYANI MASWA FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/05/mwenge-wa-uhuru-kupitia-miradi-34-yenye.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa