• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Moto Wateketeza Maduka Manane Lamadi Mkoani Simiyu

Posted on: June 3rd, 2018

Moto ambao hadi sasa chanzo chake hakijafahamika umeteketeza maduka nane , stoo pamoja na mali za wafanyabiashara  ambazo thamani yake haijafahamika, katika Mji mdogo wa Lamadi wilaya ya Busega Mkoani Simiyu , usiku wa tarehe 02 Juni.

Akizungumzia jinsi moto huo ulivyoanza mmoja wa wakazi wa Lamadi aliyeshuhudia tukio hilo, Bw. John Balele amesema moto ulianza kuwaka katika moja ya chumba cha duka majira ya saa mbili usiku na baadaye ukaanza kusambaa katika vyumba vingine lakini hawakuweza kufahamu chanzo chake maana vyumba vyote vilikuwa vimefungwa.

“Huu moto umetokea majira ya saa mbili hivi tulivyouona tukapiga simu polisi, askari polisi wakaja na askari wa zimamoto, watu wa Zimamoto wamejitahidi kuwahi kufika na wametusaidia sana kutuelekeza namna ya kukabiliana na moto huu tukafanikiwa kuuzima na kuokoa baadhi ya mali  japo mali nyingi zimeteketea; binafsi nawashukuru sana wananchi wenzangu wa Lamadi kwa moyo wao wa kujitolea” alisema John Balele.

Diwani wa kata ya Lamadi, Mhe. Laurent Bija amewashukuru wananchi kwa namna walivyojitoa kushirikiana na jeshi la polisi na kikosi cha Zimamoto na uokoaji katika kuukabili moto huo na kulinda baadhi ya mali zilizookolewa kwa uaminifu .

Aidha, Diwani huyo ametoa pole kwa wafanyabiashara ambao mali zao zimeteketea na akatoa wito kwa wafanyabiashara wote katika Kata hiyo kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika maeneo yao ya biashara, ili viweze kuwasaidia katika hatua za awali za kukabiliana na moto pindi unapotokea.

Akizungumza wananchi wa Lamadi waliojitokeza kuzima moto huo wakishirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Polisi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewapa pole wafanyabiashara ambao wamepoteza mali zao katika ajali hiyo ya moto na akawashukuru wananchi wa Lamadi kwa ushirikiano na uaminifu waliounesha wakati wa kuzima moto huo.

Mtaka amesema kwa kuwa chanzo cha moto huo hakijafahamika Serikali kupitia TANESCO na Zimamoto itaendelea kutafuta na kubaini chanzo na tarehe 03 Juni, 2018 Serikali itafanya tathmini kujua madhara yaliyosababishwa na moto huo.

“ Nawapa pole wananchi wa Lamadi bado hatujajua chanzo hasa, wenzetu wa TANESCO na Zimamoto watatusaidia kujua chanzo, kuhusu madhara kwa kuwa sasa ni usiku kesho Serikali itafanya tathmini ili na sisi tuone namna ya kuzungumza na wenzetu wa benki na kuona busara gani itumike kuwasaidia wafanyabiashara waliokopa namna ya kurejesha, wakati wanajipanga upya” alisema

Mkuu huyo wa Mkoa pia ametoa wito kwa Taasisi za Bima hapa nchini kupanua wigo na kuwafikia wafanyabiashara na kuona namna sahihi ya kuwa msaada kwao pale wanapokutana na majanga yasiyoepukika yakiwemo ya moto, huku akisisitiza wafanyabiashara kuchukua tahadhari ya moto ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vifaa vyote vya umeme vimezimwa wanapofunga biashara zao.  

Katika hatua nyingine  ametoa wito kwa Jeshi la Zimamoto kuendelea kutoa elimu ya majanga ya moto hasa kwenye maeneo ya masoko ili waweze kuchukua tahadhari ya moto na akawataka wale wanaojenga majengo ya biashara kupata ushauri wa kitaalam juu ya ujenzi wa majengo yao

Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Simiyu, Gervas Fungamali amesema Jeshi la polisi litaendelea kutoa elimu  kwa wananchi hususani juu ya umuhimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto na kuchukua tahadhari ya moto katika maeneo yao.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/06/moto-wateketeza-maduka-nane-lamadi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa