Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe.David Kafulila, amewapongeza wakurugenzi na wakuu wa wilaya 5 za Mkoa wa Simiyu (Wilaya ya Busega, Bariadi, Maswa, Itilima na Meatu) kwa kuendelea kuboresha usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusisitiza kuwa juhudi hizo ndizo zilizofanikisha mkoa wa simiyu kushika nafasi ya 4 mwaka huu 2021 kutoka nafasi ya 20 mwaka 2019 katika miradi ya Mwenge Pongezi hizo amezitoa wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
"Mimi naona fahari kuwa na timu hii ya wakuu wa wilaya na wakurugenzi.Naamini mwakani tutashika nafasi ya 1" amesema Kafulila.
“Mbali ya kupaisha mkoa huu kutoka nafasi ya 2 toka mwisho mwaka 2020 mpaka nafasi ya 2 juu katika makusanyo ya halmashauri kimkoa, leo nimepata taarifa kuwa mkoa wetu umeshika nafasi ya 4 kitaifa katika miradi ya mwenge iliyokaguliwa kulinganisha na nafasi ya 20 ambayo ilishikwa mwaka 2019. Angalia hapa Busega, taarifa ya makusanyo ya robo ya mwaka wa fedha 2020 ilikuwa asilimia 15% ya lengo, kulinganisha na asilimia 29% kwenye robo ya kwanza mwaka 2021.Hivyo inawezekana. Tuendelee kupambana kujenga mkoa wetu " alisisitiza Kafulila.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa