• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Maswa Waridhia Kaya kuchangia shilingi Elfu 50 kwa mwaka kwa ajili ya maendeleo

Posted on: May 31st, 2018

Viongozi wa wananchi, wenyeviti wa vitongoji na vijiji 120 vya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wameridhia mchango wa shilingi elfu hamsini kila kaya kwa ajili ya shughuli za maendeleo ambao utatolewa kwa mwaka, ambapo baada ya kaya kutoa mchango huo hazitachangia mchango mwingine wowote.

Hayo wameyasema katika mkutano uliofanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Mjini Maswa baina ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na viongozi wa vitongoji ,vijiji na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa, viongozi wa dini  na wananchi, lengo likiwa ni kujadili azimio lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Maswa la Uchangiaji shughuli za maendeleo hususani ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya.

“Kwanza ni  vizuri ikafahamika kwamba viongozi wa wananchi wameridhia mchango, hii habari ya nani kasema hapana ni lazima tutoe uhuru wa kutoa maoni, sidhani kama ingekuwa sahihi  tuje hapa tuamue kuwa haya ni maelekezo; lakini pili hatujasema adhabu  kuwa asiyetoa mchango huu atafanywa nini waandishi wa habari saidieni kuondoa uzushi huu kwenye mitandao” amesema Mtaka.

Mtaka amesema ni vema  ikafahamika wazi kuwa baada ya kaya kutoa  mchango huu wananchi hawatachangiswa mchango wowote, huku akisisitiza kuwa mchngo huu hautazihusu zilizo chini ya Mpango wa Kunusuru kaya Maskini TASAF III pamoja na kaya za wananchi walio katika misamaha mbalimbali ya Serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati akihitimisha mkutano huo amesema uamuzi wa kuwa na mchango huo umetokana na kuona wananchi wamekuwa wakichangishwa michango mingi ya rejareja ambayo ilikuwa ikizidi kiasi cha shilingi elfu 50,  hivyo Halmashauri ikaona ipo haja ya kuwa na mchango mmoja ambao utakuwa na unafuu.

“Huu mchango ni sawa na michango mingine ambayo Wananchi wamekuwa wakichangia siku zote kwa ajili ya shughuli za maendeleo, lakini sasa hivi Halmashauri baada ya kuona wananchi wakichangia rejareja wanachangia fedha nyingi, iliona ni vema kukawa na mchango mmoja kwa mwaka wa shilingi elfu 50” alifafanua Mtaka.

Awali akitoa ufafanuzi kuhusu mchango huo Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe amesema wilaya hiyo ilifikia uamuzi wa kuwa na mchango mmoja kutokana na michango iliyokuwa ikitolewa rejareja kutokuwa na matokeo yaliyokusudiwa, ikiwa ni pamoja na miradi iliyokusudiwa kujengwa na fedha za michango hiyo hususani miundombinu yal elimu na Afya kutokamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Erasto Mbigili Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbalagane amesema  anaunga mkono wazo la kuwa na mchango mmoja kwa mwaka ambao utawarahisishia Wenyeviti wa Vijiji na vitongoji na kuwaondolea kero ya kwenda kila mara kuwasumbua wananchi kuomba michango.

Naye John Dalawida Mwenyekiti Kitongoji cha Matale amesema anaunga mkono wazo hilo ambalo limeanzia kwa madiwani ambao ni wawakilishi wao na anaamini litasaidia ukamilishaji wa maboma ya vyumba vya madarasa na zahanati waliyoanza kujenga ili kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya wilayani Maswa.

Jeremia Shigala Diwani wa kata ya Zanzui amesema Baraza la madiwani lilizimia kuja na mchango huo baada ya wataalam wa Halmashauri kuonesha mchanganuo kuwa wananchi wilayani humo wamekuwa wakichangia wastani wa shilingi elfu 70 kwa mwaka,  hivyo alilipokea na kuahidi kwenda kuwaelimisha wananchi  juu ya umuhimu wa mchango huo wa mara moja.

Katika Mkutano huo viongozi wa Chama na Serikali walitoa michango yao ya fedha taslimu, ahadi na vifaa vya ujenzi ili kuuunga mkono wazo la ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya katika wilaya ya Maswa, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu aliahidi kutoa shilingi 1,000,000/=, Mkuu wa wilaya hiyo aliahidi kutoa shilingi 500,000/= Mkurugenzi wa Halmashauri aliahidi kutoa shilingi 500,000/= na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) akaahidi kutoa jumla ya mabati 500 kama mchango wake.

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/05/maswa-waridhia-kaya-kuchangia-shilingi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa