• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Makamu wa Rais Mgeni Rasmi Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa Mkoani Simiyu

Posted on: March 2nd, 2020

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo Kitaifa yatafanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Mjini Bariadi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Maadhimisho haya yanaongozwa na kauli Mbiu "Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na ya baadaye"  ambapo yataanza tarehe 02 Machi 2020 mpaka tarehe 08 Machi 2020.

"Katika Maadhimisho haya tunawatarajia wageni mbalimbali na shughuli mbalimbali kufanyika; mathalani kuanzia Tarehe 02 Machi 2020 maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wanawake zitaoneshwa, wajasiriamali kutoka maeneo yote nchini wamethibitisha kushiriki pia kutakuwa na upimaji kwa magonjwa mbalimbali ya Wanawake,"

"Siku ya tarehe 06 Machi 2020 kutakuwa na Jioni ya mwanamke ambapo wake za Viongozi waliopo madarakani na wastaafu na Watendaji mbalimbali wa Taasisi watashiriki; mpaka sasa Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya nne, Mama Tunu Pinda, Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania na viongozi mbalimbali Wanawake wamethibitisha kushiriki, wakiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu," alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kushiriki katika shughuli zote zitakazofanyika katika Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa na kilele chake ambazo zitafanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Katika hatua nyingine Mtaka amesema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku tatu Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 06 Machi 2020 hadi 08 Machi  2020.

Amesema tarehe 06 Machi, 2020 Mhe. Makamu wa Rais atafungua Tawi la Benki ya NMB katika Kata ya Nyashimo makao Makuu ya Wilaya ya Busega na baadaye kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Tawi la Chuo cha Usimamizi (IFM), katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi.

Ameongeza kuwa tarehe 07 Machi, 2020 Mhe. Makamu wa Rais atafungua Ofisi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ya Mkoa na siku hiyo hiyo ataweka jiwe la msingi Ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichopo Kata ya Somanda.

"Nitumie nafasi kuwaomba Wananchi wa Mkoa wa Simiyu hususani katika maeneo yote ambayo Mhe. Makamu wa Rais atapita kujitokeza kwa wingi kumsikiliza kwa kuwa katika maeneo yote ambayo Mhe. Makamu wa Rais atafungua na kuweka mawe ya msingi miradi, atazungumza na wananchi, " alisema Mtaka.

Mhe. Makamu wa Rais atahitimisha ziara yake Mkoani Simiyu tarehe 08 Machi kwa kuwaongoza wananchi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa.

MWISHO

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa