Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Agosti Mosi, 2019 amezindua mkakati wa udhibiti wa upotevu wa mazao wenye lengo la kumsaidia mkulima namna ya utunzaji Bora wa mazao baada ya mavuno.
Mama Samia amezindua mkakati huo katika ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Nane Name Kitaifa, uliofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Amesema upotevu wa mazao ni moja ya changamoto zinazowakabili wakulima na kupelekea kuwa na tija ndogo huku akizitaja changamoto nyingine kuwa ni matumizi hafifu ya mbolea, kutopata mbegu na viuatilifu kwa wakati na vilivyo bora na kutotumia kanuni bora za kilimo.
Aidha, Mhe. Makamu wa Rais ametoa wito kwa Taasisi za Umma, binafsi, vyama vya ushirika na Taasisi za kiraia zinzojishughulisha na Maendeleo ya Kilimo kuhakikisha wanarekebisha kosoro zilizopo na kutoa elimu bora na kutosha inayojibu changamoto hizo.
Katika hatua nyingine Mhe. Makamu wa Rais ametoa rai kwa watafiti wote nchini kutoa matokeo ya tafiti zao kwa maafisa ugani na wadau wengine ili wakulima wanufaike na matokeo hayo.
Akizungumzia mkakati wa kudhibiti upotevu wa mazao miaka 10, Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga amesema lengo la serikali ni kuhakikisha inapunguza upotevu wa mazao kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema dhamira ya mikoa inayounda Kanda ya Nanenane ya Ziwa Mashariki ni kuvifanya viwanja vya maonesho ya Nanenane Nyakabindi kuwa ni mahali patakapojibu kwa vitendo sera za wizara ya kilimo na pawe mfano kwa wananchi kujifunza Kilimo Biashara.
Pia ametoa wito kwa wanunuzi wa pamba kuendelea kununua pamba kwa bei elekezi ya shilingi 1200 na taasisi za fedha kutoa fedha kwa wanunuzi pamba ya wakulima inunuliwe, huku akiiomba Serikali kuridhia sehemu ya fedha ikakatwa fedha hiyo iweze kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha nguo kwa kushirikiana na wadau wengine ili kuwa na soko la uhakika la pamba.
Mkoa wa Simiyu uko tayari kutekeleza agenda ya ujenzi wa kiwanda cha nguo kupitia Vyama vya Ushirika vya Msingi, Chama Kikuu cha Ushirika (SIMCU) na wawekezaji walio ndani ya mkoa huku akibainisha kuwa
Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanafanyika kwa mara ya pili mfululizo sasa katika Kanda ya Ziwa Mashariki inayoundwa na Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga, yakiwa na Kauli Mbiu isemayo Kilimo, Mfugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi”.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/08/makamu-wa-rais-azindua-mkakati-wa.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa