• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Makampuni 12 Kuanza Kununua Pamba kwa Bei Elekezi 1200

Posted on: July 1st, 2019

Baada ya kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau wa pamba mkoani Simiyu jumla ya makampuni 12 yamekubali kuingia sokoni kunua pamba ya wakulima kwa bei elekezi ya shilingi 1200.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kufunga kikao maalum cha kujadili mstakabali wa ununuzi wa pamba katika mkoa wa Simiyu, ambapo pia ilielekezwa kuwa makampuni yaliyokubali kununua pamba kwa wakulima yazingatie sheria na taratibu na yawalipe wananchi fedha zao  kwa wakati.

Mtaka ameyapongeza makampuni yote yaliyokubali kuingia kununua pamba huku akiahidi kutoa msaada kwa wafanyabiashara wanaokutana na changamoto ya upatikanaji wa fedha kutoka katika taasisi za fedha na kuwahakikishia kuwa kila atakayehitaji msaada atamsaidia ili apate fedha.

Aidha, Mtaka amesema yeyote atakayebainika kufanya udanganyifu katika mizani achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria huku akiutaka wakala wa vipimo kusimamia na kuhakikisha mizani hazichezewi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi(AMCOS).

“ Kama kuna wakati Wakala wa Vipimo unahitaji kuwa na saa nyingi za kufanya kazi ni sasa kama magari hayatoshi waombe tutawapa na kama watumishi hawatoshi omba watalaam kutoka katika maeneo mengine, kama kuna mtu atakutwa amefanya udanganyifu katika mizani kwenye vyama vya ushirika achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria” alisema Mtaka.

Kwa upande wao Wanunuzi wa pamba mkoani SIMIYU wameiomba serikali kuondoa tozo zote zilizopo kwenye utaratibu wa ununuzi wa pamba, ili kupunguza hasara watakayopata kwa kununua pamba kwa Bei elekezi ya shilingi 1200 kwa kilo kutokana na bei ya soko la dunia kushuka, jambo ambalo lililofafanuliwa na Katibu Tawala Mkoa, Bw.Jumanne Sagini kuwa tozo hizo ni jambo la kisera na kisheria nchini hivyo haliweze kufanyiwa maamuzi na mkoa.

Katika hatua nyingine baadhi ya wanunuzi wa pamba wakapendekeza kuanzishwa kwa viwanda vya nyuzi na nguo ili kuongeza thamani ya Pamba na kuondokana na utegemezi wa bei ya soko la dunia.

“Tukisema mwaka huu tutoe tozo fulani na mwakani tutatoa nyingine tena, hiyo haitakuwa tiba kwenye bei ya soko la dunia, Tiba pekee ya kulinusuru zao la pamba ni kuwekeza kwenye viwanda vya nyuzi na nguo na hilo tunaliweza, tuwekeze sisi Wanasimiyu viwanda vijengwe Simiyu” alisema Mnunuzi wa Pamba Gungu Silanga.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe, Festo Kiswaga amewataka wanunuzi wote kuzingatia sheria wakati wakinunua pamba ya wakulima na akasisitiza kuwa wale watakaokiuka sheria ikiwa ni pamoja na kununua pamba usiku watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Baadhi ya Makampuni yaliyokubali kuingia kununua pamba mkoani Simiyu ni pamoja na Alliance Ginneries Limited, NGS, MWATEX, GAKI, OLAM, SM na Vitrex

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/07/makampuni-12-kuanza-kununua-pamba-kwa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa