• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

MADC, WAKURUGENZI MKOANI SIMIYU WAGIZWA KUUNDA TIMU KUJIRIDHISHA JUU YA WANAFUNZI WANAODAIWA KUWA MAMLUKI

Posted on: November 28th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani humo kuunda timu zitakazopitia na kujiridhisha juu ya  majina ya wanafunzi 633 waliotajwa kuwa Mamluki na kuondolewa shuleni kwa kukosa sifa za kusoma shule za sekondari za Serikali kutokana na sababu mbalimbali.

Agizo hilo amelitoa jana katika Shule ya Sekondari Nkoma wilayani ITILIMA kwenye  kikao chake na viongozi, watendaji wa Serikali na wazazi wa baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo walioondolewa katika mfumo wa Serikali kutokana na kutumia majina yasiyo yao, kukosa fomu  za TSM 9 , kukosa vibali vya kukariri/kurudia kidato na vibali vya uhamisho.

Mtaka amesema timu hizo zitakazoundwa kwa kila Wilaya zifuatilie na kujiridhisha kwa kupitia majina yote  pamoja na sababu za wanafunzi hao kuitwa Mamluki na kuondolewa katika mfumo wa Serikali zilizoanishwa, ambapo amebainisha kuwa watendaji wa Idara ya Elimu watakaobainika kusababisha kwa uzembe wanafunzi hao kuondolewa shuleni watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Ameongeza kuwa Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Elimu Sekondari waitishe vikao na wanafunzi hao na wazazi wao, ili wazungumze na kuwaeleza hatua zitakazochukuliwa baada ya kujiridhisha, baadaye taarifa ya kila wilaya iwasilishwe mkoani.

“Kufikia Ijumaa wakuu wote wa Wilaya na Maafisa Elimu wawe wamekutana na wanafunzi waliopata matatizo hayo,wazazi wao na watoto wote waitwe kutoa ushuhuda wa nini kimesababisha wao kuitwa mamluki na kurudishwa nyumbani,  wakishajiridhisha watuletee hiyo taarifa na sisi Mkoa tutaipitia na kutoa maelekezo; tunaweza kusema wanafunzi 633 ni mamluki kumbe umamluki wa baadhi ya wanafunzi umesababishwa na  uzembe wa Watendaji wetu.” alisisitiza Mtaka.

Aidha baada ya kusikiliza hoja za baadhi ya  wanafunzi walioondolewa katika mfumo wa shule za Serikali pamoja na  wazazi wao shuleni Nkoma na kubaini kuwa baadhi ya sababu zilizopelekea wanafunzi hao kuondolewa zimechangiwa na uzembe wa baadhi ya Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Wilaya na Wakuu wa Shule Mtaka ameagiza wanafunzi hao warudishwe shuleni mara moja.

“Kuna wanafunzi hapa Nkoma tumewasikiliza kesi zao wapo ambao walipaswa kurudia darasa , taratibu za upatikanaji wa kibali cha kurudia darasa kama wanafunzi pamoja na wazazi wamefanya, lakini inaonekana kuna uzembe kati ya Wakuu wa Shule na Idara ya Elimu Wilaya, maagizo ya Serikali ya Mkoa vibali vya wanafunzi hao kufikia tarehe 29/11/2017 viwe vimetolewa na warudishwe shuleni” amesema Mtaka.

Sanjari na hilo Mtaka ameagiza wanafunzi wote wanaosoma shule za Sekondari kwa kutumia majina ya watu wengine waondolewe katika mfumo wa shule za Sekondari za Serikali na akatoa wito kwa wazazi wao kuwapeleka katika shule binafsi au katika utaratibu wa utahiniwa binafsi (QT) ili wafanye mitihani kama watahiniwa binafsi (Private Candidates).

Baadhi ya wanafunzi waliondolewa katika mfumo wa Shule za Serikali katika Shule ya Sekondari Nkoma Wilayani Itilima kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya kutumia majina ya watu wengine wamesema wako tayari kuendelea na masomo ikiwa watapata nafasi katika shule binafsi, ambapo wazazi wao pia wamesema wako tayari kuwapeleka watoto wao katika shule binafsi ili kuwasaidia wafikie malengo yao.

“ Nilipata taarifa kuwa mwanangu ameondolewa shuleni kwa sababu anatumia jina la mtu mwingine na nimeshaanza kutafuta nafasi kwenye shule za binafsi ili aendelee na masomo kwa sababu alikuwa anafanya vizuri darasani, kwa mfano muhula uliopita aliongoza” alisema Sumuni Daudi mmoja wa wazazi walioshiriki kikao na Mkuu wa Mkoa.

 Naye Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga ameomba kuwepo na darasa maalum kwa wanafunzi watakaobainika kuwa siyo halali  waandaliwe utaratibu wa  kufundishwa na baadaye wafanye mitihani  kama watahiniwa wa kujitegemea ili waweze kutimiza ndoto zao.

Wanafunzi waShule ya Sekondari Nkoma Wilayani Itilima pamoja na wazazi wao wakimsikiliza Mkuuwa Mkoa katika kikao maalum kilichofanyika shuleni hapo jana.

Wanafunzi waShule ya Sekondari Nkoma Wilayani Itilima pamoja na wazazi wao wakimsikilizaMkuuwa Mkoa katika kikao maalum kilichofanyika shuleni hapo jana.

Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe.Njalu Silanga akichangia hoja katika kikao kilichoitishwa naMkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuzungumza na viongozi wa Serikali,wanafunzi walioondolewa shuleni kutokana na sababu mbalimbali pamoja na wazazi wao.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi akifuatilia kwa makini hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuzungumza na viongozi wa Serikali , wanafunzi walioondolewa shuleni kutokana na sababu mbalimbali pamoja na wazazi wao wilayani humo.

Mmoja wawanafunzi walioondolewa shuleni kutokana na kukosa sifa za kusoma katika shuleza Sekondari za Serikali akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa na viongozi wenginewa Serikali juu sababu ya kuondolewa shuleni.

Mmoja wa wazaziwa wanafunzi walioondolewa shuleni kutokana na kukosa sifa za kusoma katika shule za Sekondari za Serikali akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine wa Serikali katika kikao kilichofanyika Shule ya Sekondari Nkoma wilayani Itilima kujadili suala hilo.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa