• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Kongamano la Maombi Lafanyika Mkoani Simiyu, Kuuombea Mkoa

Posted on: January 12th, 2022

Kongamano la kuuombea Mkoa wa Simiyu limefanyika hivi karibuni kuuombea Mkoa, ili uweze kuepukana na Majanga mbalimbali kama vile Ukame, Magojwa, Misiba na ajali.Kongamano hilo la maombi limefanyika katika Viwanja vya Halmashauri ya Mji Bariadi.

 Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amesema ili kupata mafanikio yoyote yale duniani ni lazima kumtanguliza Mungu, sababu ya uzito wa jina lake kwenye hatma yetu,kwani yapo mahubiri ambayo mwenyezi mungu anayahubiri katika maisha yetu kwa vitendo.Upo uwezekano wa sisi kupata neema kwa sababu ya wachache walio na Mungu au kupata matatizo kutokana na wenzetu wachache tulionao.katika kusisitiza hilo Mhe Kafulila alitoa mfano wa Abraham wa kwenye masimulizi ya biblia ambaye alimuomba mwenyezi Mungu na kumsihi zaidi ya mara tatu asiliangamize jiji la Sodoma na Gomora naye Mungu alisikiliza sihi na maombi ya Abrahamun zaidi ya mara tatu.  Mhe. Kafulila aliendelea kutoa mfano wa  Yona ambaye kwa kukimbia jukumu alilopewa na Mwenyezi Mungu la kwenda kuwahubiria watu wa Ninanwi alisababisha balaa nadani ya  chombo na bahari kuchafuka kiasi cha kwamba chombo kilitaka kuzama, Wakati hali hii inatokea kila mtu alliyekuwa ndani ya chombo alisali kwa Mungu wake na baada ya Yona kutupwa baharini na kumezwa na samaki chombo kilitulia na kisha Yona kutapikwa katika jiji la Tarshishi.Yote haya yaonyesha kwamba hata tuwe katika hali gani wa kumtegemea ni Mwenyezi mungu nmaye  husikia sala za watu wake.

 Mhe. Kafulila ameeleza kuwa tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, majanga yamekuwa yakitokea mara kwa mara mkoani humo hususani vifo vya viongozi mbalimbali na hata kifo cha msaidizi wake wa karibu,aidha magonjwa, ukame na aksidenti za barabarani kutia ndani ajali iliyotokea 11/1/2022 ambayo ilisababisha vifo vya watu 15 kufikia leo, ni majanga ambayo yameupata mkoa wetu kwa kipindi kifupi cha wakati

."Hivyo nimeona ni vyema sisi sote kwa umoja wetu bila kujali dini wala itikadi tukutane kwa pamoja na kumsihi Mwenyezi Mungu kupitia haya maombi maalum atuepushe na majanga haya yote pamoja na kushukuru kwa baraka ambazo tayari ametupatia". Amesema Kafulila.

 Kongamamo hilo limeshirikisha viongozi wa Dini zote mkoani Simiyu, wananchi na wanakwaya kutoka katika dini zote.Katika kongamano hilo kwaya mbalimbali zilitumbuiza zikiwa na ujumbe wa kumsihi Mwenyezi Mungu atuepushe na majanga yote na kumshukuru kwa baraka ambazo ameupatia Mkoa wa Simiyu.Pamoja na kuuombea mkoa wa Simiyu,viongozi wa dini walimuombea Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan na kumshukuru kwa vipaumbele ambavyo amevipa Mkoa wa Simiyu.

Viongozi wa Dini walisisitiza Amani, Umoja na Upendo pamoja na tabia ya  kumtegemea Mwenyezi Mungu kwani Mungu asipoijenga Nyumba waijengao wafanya kazi bure. Aidha Viongozi hao walisisitiza pamoja na kuwa na dini mbalimbali cha muhimu ni upendo ambapo tukiwa na upendo ni rahisi kuvumiliana na hivyo kutokeza amani.

Kila Kiongozi wa Dini alipewa eneo la kuliombea ikiwa pamoja na amani na upendo, magonjwa, ukame, ajali na ustawi wa viongozi.

 "Aidha niwashukuru viongozi wote wa dini kwa jinsi mlivyojipanga na kuongoza maombi haya sina cha kuwalipa zaidi niseme ahsanteni sana.Pamoja na kuwashukuru Viongozi wa dini zote,pia niwashukuru Wanakwaya ambao nanyi ni sehemu ya dini kwani kwa nyimbo zenu mmetoa mahubiri tosha".Amesisitiza Kafulila.

Mwisho.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa