• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Kiwanda cha Ushonaji Kuajiri Vijana na Wanawake Simiyu

Posted on: August 16th, 2018

Kukamilika kwa kiwanda cha ushonaji katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi kutasaidia kuongeza ajira, ujuzi na vipato vya wananchi wa Simiyu hususani wanawake na vijana.

Kiwanda hicho kinakadiriwa kujengwa kwa fedha kiasi cha shilingi milioni 85 hadi kukamilika kwake ambapo itatoa pia fursa kwa wakazi wa mji wa Bariadi na Mkoa mzima kwenda kujifunza ushonaji na ubunifu wa mitindo mbalimbali ya nguo ambayo baadae wataweza kujiajiri na kujiongezea kipato.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa kiwanda hicho  mbele ya kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 Ndg. Charles Kabeho  kabla ya kuweka jiwe la msingi kiwanda hicho ,Mhandisi wa Halmashauri ya Mji Samwel Msolini amesema Halmashauri ilipokea msaada wa vyerehani 50,  kutoka Serikali ya Jamhuri ya China, vyerehani 25 vikiwa vya umeme na vingine 25 ni vya kawaida.

Ameongeza kuwa baada ya kupokea msaada huo Halmashauri imeamua kuanzisha Kiwanda hicho ili kuviwezesha kutumika na hatimaye Halmashauri ipate mapato, kutoa ajira kwa wananchi na wananchi kupata huduma za mavazi yenye kiwango.

  

“”Lengo la Ujenzi wa Kiwanda cha Ushonaji ni kwa ajili ya kushona nguo kwa mahitaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na nguo zinazovaliwa  kwenye sherehe mbalimbali, sare za shule na maeneo ya kazi, mradi huu ukikamilika utaongeza mapato ya Halmashauri, kutoa ajira kwa wananchi na wananchi watapata huduma ya mavazi” alisema Msolini..

 

Aidha,  akiweka jiwe la msingi katika kiwanda hiki, kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho amefurahishwa sana na akapongeza Halmashauri kwa kubuni mradi huo ambao amesema utakuwa na manufaa kwa wananchi na Halmashauri.

“Kiwanda hiki  kitawasaidia wajasiriamali wanaojihusisha na masuala ya ushonaji  kupata kipato, kitawasaidia wananchi kujiajiri wenyewe, lakini pia Halmashauri nayo itapata mapato” alisema Charles Kabeho..

Angello Michael mkazi wa mji wa Bariadi alisema kiwanda hicho kitasaidia vijana na wanawake wengi ambao hawana kazi za kufanya na kubadilisha maisha na vipato vyao kwa baadaye.

Katika hatua nyingine Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 amewapongeza Wananchi na Viongozi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa namna walivyoshirikiana katika ujenzi wa Miundombinu ya Elimu katika Shule ya msingi Kilulu na akatoa wito wananchi kwenda kujifunza ujenzi wa majengo mazuri yenye kiwango kwa gharama nafuu.

Aidha Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri Mji wa Bariadi,  pamoja na kuweka Jiwe la Msingi la kiwanda cha ushonaji, umepitia miradi mingine katika Sekta ya Elimu, Afya, Mazingira, Sekta Binafsi  na Ujenzi.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/kiwanda-cha-ushonaji-kuajiri-vijana-na.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa