• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Kilo 145,000 za Choroko Zauzwa Mnada wa Kwanza Simiyu

Posted on: March 2nd, 2021

Takribani kilo 145,000 za zao la choroko mkoani Simiyu zimeuzwa kupitia mnada uliofanyika kwa mara ya kwanza katika ghala lililopo kiwanda cha zamani cha kuchambua pamba cha Sola wilayani Maswa, ambapo kilo moja ya choroko imeuzwa kwa shilingi 1578 kwa kilo( kwa bei ya mnada) na mkulima kulipwa shilingi 1610 kwa kilo baada ya kupunguzwa kwa baadhi ya tozo.

Akizungumzia mnada huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema bei hiyo ya choroko kwa njia ya mnada inamkomboa mkulima na itamsaidia kuona faida na tija zaidi ya kilimo ikilinganishwa na bei ya awali ambayo mkulima alikuwa akilipwa shilingi 800 mpaka shilingi 1200 kwa kilo.

“Bei ya leo ya mnada ilikuwa shilingi 1578 kwa kilo ambayo kwa maoni ya wakulima ina faida, lakini Halmashauri kwa kushirikiana na ushirika wameongeza shilingi 32 kwa kilo ili kumsaidia mkulima kufanya maandalizi ya msimu unaofuata wa mazao mengine na shughuli nyingine, kwa hiyo leo mkulima amepata shilingi 1610 kwa kilo,” alisema Mmbaga.

Aidha, Mmbaga amewahakikishia wakulima usalama wa mazao yao yatakapopokelewa katika maghala makuu kwa kuwa watunza maghala wamekata bima zote ikiwepo bima ya moto na wizi kwa ajili ya kubeba dhamana ikiwa kutatokea majanga au wizi.

Wakati huo huo Mmbaga ametoa wito kwa wakulima kulima kilimo biashara ili waweze kupata faida na kuona tija katika kilimo chao huku akiwasisitiza kutumia fedha zao vizuri kwa kuwekeza kwenye shughuli za maendeleo ili waweze kutatua mahitaji mbalimbali ya kijamii.

Katika hatua nyingine Mmbaga ametoa wito kwa Wafanyabiashara kutoka mikoa yote nchini kushiriki katika minada ya ununuzi wa choroko katika maghala yaliyopo mkoani hapa na kuwahakikishia ushirikiano wakati wowote watakapohitajika.

Bw. Daniel Mipawa ambaye ni mkulima kutoka Chama cha ushirika cha Msingi cha Nhaya amesema uuzaji wa choroko kupitia mnada ameupokea vizuri kwa kuwa umekuwa msaada kwenye suala la bei maana wakulima wamekuwa wakiwauzia choroko baadhi ya wafanyabiashara shilingi 800 mpaka shilingi 1200.

Naye mfanyabiashara Ibrahim Musa akizungumzia hali ya mnada na bei ya choroko amesema “Bei ya mnada wa leo wa choroko ya shilingi 1578 kwa kilo ilikuwa haitulipi lakini tumekaa na viongozi wa serikali wameamua kutupunguzia baadhi ya tozo, kwa kuwa wametupunguzia baadhi ya tozo na kuturudishia gharama za usafiri sasa hivi tutaenda vizuri.”

Kwa upande wake Msimamizi wa ghala kuu Maswa, Bw. Abdallah Ngozi amesema mnada wa choroko umeenda vizuri na kushauri wakulima pamoj na kuwa na nafasi ya kuamua kuuza au kutokuuza kulingana na bei ya mnada wa siku husika wawe makini kwa kuwa wanaweza kukataa kuuza na bei ikashuka zaidi ya ile ya awali

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2021/03/kilo-145000-za-choroko-zauzwa-mnada-wa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa