• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Kaya 6120 za Walengwa wa TASAF Mkoani Simiyu Zalima Pamba Ekari 8712 Msimu wa mwaka 2017/2018

Posted on: April 11th, 2018

Kaya 6120 sawa na asilimia 52 ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu zimewezeshwa kulima pamba ekari 8712 katika Msimu wa mwaka 2017/2018 kwa kutumia fedha za uhawilishaji. 

Hayo yalibainishwa na  Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu Bw. Nyasilu Ndulu wakati wa kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi juu ya mpango huo kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.

Nyasilu amesema pamoja na kulima pamba walengwa wa mpango huo katika Wilaya ya Bariadi na wilaya nyingine Mkoani Simiyu kupitia fedha za uhawilishaji (wanazopewa) wamefanikiwa kujenga nyumba, kufuga, kuanzisha biashara ndogo ndogo na kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).

Ameongeza kuwa tangu kuanza kwa zoezi la uhawilishaji chini ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini awamu ya tatu mwaka 2015 hadi sasa,  tayari awamu 17 za malipo zimekwisha fanyika kwa walengwa 37, 533 na jumla ya shilingi bilioni 28.9 zimelipwa kwa wahusika.

Amesema fedha hizo zimejumuisha ruzuku za aina mbili ikiwa ni ruzuku ya msingi na ile itokanayo na utimizaji wa mashati ya Afya na Elimu ambapo watoto 39,068 sawa na asilimia 90.3 wameweza kupata mahitaji muhimu ya shule na kukuhudhuria shuleni na watoto 51, 280 sawa na asilimia 93.1 wamepata mahitaji ya kliniki na kupelekwa kliniki.

“Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini umeweza kuwasaidia walengwa kujikwamua kutoka kwenye umaskini, wapo walioanzisha biashara, wanaolima, wanaofuga, waliojenga nyumba bora; kwa kutumia fedha hizi wanazopewa wapo ambao watoto walikuwa hawahudhurii shuleni na kliniki lakini sasa hivi mahudhurio mazuri” Alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka awali akifungua kikao amesema pamoja na mafanikio waliyoyapata walengwa, wanufaika wote waliofanya mambo ya maendeleo ni vema wakawa mfano kwa wenzao huku akiwataka wale walioshindwa kuondolewa kwenye mpango huo.

Aidha, Mtaka aliwataka walengwa wote wa mpango kuendana na malengo ya nchi ya kuelekea kwenye Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025 badala ya kuwaza kuendelea kubaki katika mpango huo.

“Mtazamo wangu mimi ni vizuri wanufaika wa TASAF waendane na Mpango wa Nchi, tunaposema tunataka kwenda kwenye Uchumi wa Kati kufikia mwaka 2025 wanufaika wa TASAF wanapaswa kujindaa kwenda kwenye uchumi wa kati, ili badala ya watu kutaka tu kuingia kwenye mpango,  tupate watu wanaotaka kutoka baada ya kupiga hatua na kutoka kwenye umaskini waliokuwa nao mwanzo” alifafanua Mtaka

Nae Bw. Fariji Mishael mtaalamu wa ufuatiliaji wa tathmini kutoka Ofisi ya TASAF Makao  makuu aliupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza mpango huo vizuri na kuomba wataalamu kuwasaidia walengwa walio kwenye maeneo yao katika  kuwashauri namna bora ya kuendesha miradi waliyoianzisha ili iwe endelevu na iweze kuwasaidia kiuchumi.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/04/kaya-6120-za-walengwa-wa-tasaf-wilayani.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa