Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewatembelea wanafunzi wa Mkoa wake walio katika Kituo cha Mashindano ya Kitaifa ya UMITASHUMTA Butimba jijini Mwanza, ambapo wapo na wenzao kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara wamekusanyika.
Akiwa kituoni hapo Sagini alizungumza na wanafunzi wanamichezo kutoka mkoani Simiyu na kutoa zawadi ya fedha taslimu shilingi 580,000 kwa wanafunzi 12 ambao wameifanya Simiyu kufanya vizuri na kupata medali 12 Sita zikiwa za shaba na sita nyingine dhahabu kwenye mchezo wa riadha katika mashindano ya UMITASHUMTA ambayo yanaendelea.
Aidha, Sagini amewapongeza wanafunzi waliofanikiwa kuufikisha mkoa wa Simiyu kwenye robo fainali katika mchezo wa mpira wa mikono (handball) na timu ya mpira wa miguu wasichana ambao walikosa nafasi moja kuelekea robo fainali.
Mashindano ya UMITASHUMTA Kitaifa yanatarajiwa kufungwa Juni 29 , 2018 na watoto wote wataanza kurudi majumbani kwao.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory amesema wanafunzi wote walioko kwenye mashindano ya Kitaifa ya UMITASHUMTA jijini Mwanza wako salama.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa