• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

JPM Anamuenzi Mwalimu Nyerere Kwa Vitendo: RC Mtaka

Posted on: October 14th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema serikali ya awamu ya tano chini ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe inamuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo hususani katika kuendeleza kazi nzuri alizozifanya.

Mtaka ameyasema hayo Oktoba 14, 2019 katika Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi, likiwashirikisha viongozi wa Serikali, wananchi na baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu, UVCCM Simiyu, UVCCM kutoka mikoa mbalimbali nchini na ngazi ya Taifa(makao makuu).

“Mwalimu amepewa heshima ya kuenziwa ninyi  kizazi hiki mnashuhudia kwa macho, wapo watu wanasimuliwa tu kuwa ile barabara inaitwa ‘Nyerere road’, lakini hamkuwepo; leo mnajua kwamba hifadhi fulani inaitwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, mnasikia Mradi mkubwa wa kufua umeme wa maji wa  J.K. Nyerere,  Mhe.Rais amemheshimisha Mwalimu kwa vitendo,” alisema Mtaka

“Mwalimu aliamini katika Watanzania kufanya shughuli za kiuchumi  ikiwemo kilimo,  ufugaji na uvuvi  na akataka waongeze thamani katika shughuli hizo; ndiyo maana Mhe Rais ameanza kufufua viwanda vya nguo, viwanda vya korosho, viwanda vya kahawa na mengine aliyoyaacha Mwalimu, “ aliongeza Mtaka.

Aidha, Mtaka amemzungumzia Mwalimu Nyerere kuwa alikuwa kiongozi wa karne mwenye utu, maono na msimamo ambaye alijua wapi anapotoka na anapotakiwa kwenda kama kiongozi na aliyewaheshimisha Watanzania.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa Vijana wa UVCCM  kuwaeleza ukweli na kuwashauri viongozi vijana ndani ya Serikali kufanya kazi zao kwa kuzingatia misingi ya uongozi na kuepukana na tabia ya kuweka urasimu wa kufikika na watu , ili viongozi hao watekeleze vema wajibu wao wa kuwatumikia wananchi na kumsaidia Mhe. Rais Magufuli katika majukumu aliyowapa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo amewataka vijana kumuenzi Hayati  Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere kwa kufanya kazi kwa bidii, ili wajiletee maendeleo kwa kuwa Mwalimu aliamini kuwa kazi ni kipimo cha uhai.

Naye Kaimu Katibu Idara ya Mahusiano ya Kimataifa na Vyuo Vikuu, Bi Asha Feruz amesema kwa kuwa vijana wengi wamezaliwa wakati Hayati Baba wa Taifa,Mwl. Julius K. Nyerere akiwa amefariki ni vema vijana hao wakasoma  vitabu, ili wajue historia ya mwalimu na waasisi wengine wa Taifa la Tanzania.

Mmoja wa Wajukuu wa Mwalimu Nyerere Chifu Edward Magige amesema pamoja na Watanzania kuendelea kukumbuka na kuenzi mambo mazuri yaliyofanywa na Hayati Mwalimu Nyerere ni vema pia wakaukumbuka mchango wa Mama Maria Nyerere katika kazi zilizofanywa na mwalimu.

Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu Silanga ametoa wito kwa Vijana hapa nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura, ili waweze kuitumia vema haki yao kuchagua viongozi bora ikiwa ni namna mojawapo ya kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuchagua viongozi watakaosimamia misingi ya uongozi aliyoiweka.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII TAFADHALI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/10/jpm-anamuenzi-mwalimu-nyerere-kwa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa