Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga ametoa wito kwa Taasisi za Fedha kuhakikisha kuwa zinawafikia wakulima katika kuwezesha shughuli za kilimo ili kuongeza mchango wa kilimo katika pato la Taifa, upatikanaji wa chakula na ajira kwa Watanzania wengi, ambapo mpaka sasa takribani asilimia 65 hadi 75 wameajiriwa au kujiajiri kupitia kilimo.
Waziri Hasunga ameyasema hayo wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya Taasisi za fedha katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea, Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Amesema nchi inaweza kutoka hapa ilipo na ikasogea kwa haraka ikiwa kilimo kitawezeshwa ipasavyo kwa kuwa kilimo kikiwezeshwa kinaweza kuongeza mchango wake katika pato la Taifa.
“ Imani yangu ni kwamba nchi hii inaweza kutoka hapa ilipo kama tutakiwezesha kilimo kina uwezo wa kuongeza mchango wake kwenye pato la Taifa, upatikanaji wa fedha za kigeni, usalama wa chakula, kutoa ajira kwa watu wengi ambapo mpaka sasa hivi tuna karibu asilimia 65 hadi 75 wameajiriwa kwenye kilimo” alisema Mhe. Hasunga.
Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kufanya mabadiliko makubwa ya kuihamisha Sekta ya Kilimo kutoka kwenye kuwa sekta kujikumu na kuwa mhimili wa kweli wa ujenzi wa uchumi wa nchi na uchumi wa viwanda.
Aidha, amesema pamoja na kuwawezesha wakulima ni vema Taasisi za fedha zikatambua nafasi yake katika kuwawezesha mitaji wamiliki wa viwanda vinavyoongeza thamani mazao ya kilimo ili viweze kujengwa viwanda vya kuongeza thamani mazao mbalimbali.
Kwa upande wake Meneja wa NMB Kanda Magharibi, Bw. Sospeter Magesse amesema Benki hiyo tayari inafanya kazi na wakulima na akamhakikishia Mhe. Waziri kuwa itajipanga kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha inawafikia na kuwawezesha wakulima wengi zaidi.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/08/hasunga-azitaka-taasisi-za-fedha.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa