• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Halmashauri Zote Ingeni Mkoa wa Simiyu- Naibu Waziri Tamisemi(afya)

Posted on: December 22nd, 2021

Wito huo umetolewa leo na Mhe.Dkt.Festo Dungage Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serilkali za Mitaa (TAMISEMI-AFYA), mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19 Mkoa wa Simiyu.

Mhe.Dugange,amepongeza Sekretarieti ya Mkoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na viongozi wote wa Mkoa wa Simiyu,kwa kazi nzuri wanayofanya.

"Hongera kwa kazi nzuri sana mnayofanya mkoa wa Simiyu. Hatua ya  ujenzi wa madarasa kufikia 85%, hiyo ni hatua kubwa sana. Lengo la Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha kwamba watoto wetu wanaoingia kidato cha kwanza 2022, wote wanaingia darasani kwa pamoja , hivyo hakutakuwa na uchaguzi wa kuingia kidato cha kwanza kwa mara ya pili yaani (second Selection).

Serikali ya Awamu ya sita imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 15000 kati ya hayo  madarsa 12000 ni kwa ajili ya shule za sekondari na  madarasa 3000  kwa ajili ya shule za msigi.Mkoa wa Simiyu umepatiwa shule 380.

Kuhusa sekta ya afya pongezi kwako Mkuu wa Mkoa, RHMT na RMO, kwani sekta hii ilikuwa na changamoto sana, mikataba ambayo inatoa viwango vya upimaji  utendaji kazi (Key Performance Indicator - KPI) na vikao vya kila robo mwaka ni ubunifu wa hali ya juu kwani inaleta uwajibikaji Kabla ya kuwa Naibu Waziri nilikuwa Mwanasimiyu/mganga Mkuu na hivyo namba yangu simu yangu ilitumika kupokea malamiko mbalimbali ya wanasimiyu.Kipindi cha nyuma kulikuwa na malalamiko  mengi sana ila ndani ya miezi 6 sijapata malalamiko yeyote.

"Asilimia 95 ya huduma za afya hutolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambzo zipo chini ya TAMISEMI. Niwapongeze sana Mkoa wa Simiyu kwani  kwa kipindi cha miezi sita  mlianza matumizi ya mfumo wa GoThomis, na   65% ya vituo vyenu vya afya vinatumia mfumo huo  kwa  ajili ya kukusanya mapato. Kama aliyoeleza mkuu wa Mkoa  mfumo huo umewasaidia kuongeza mapato kutoka Tsh.200mln–600mln. Makusanyo haya yanasaidia sana kuacha utegemezi toka Serikali kuu au wafadhili. Hivyo ni vyema Halmashauri zote ziige mkoa wa Simiyu" amesema Mhe. Dugange .

Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amemshukuru Mhe. Dugange kwa kutembelea mkoa wa Simiyu,na kumhakikishia kuwa ujenzi wa madarasa ambao umefikia  85% utamalizika kwa wakati. Kwa upande wa sekta ya afya Mhe. Kafulia amemfahamisha Naibu Waziri Tamisemi /afya kuwa mafanikio katika sekta ya afya yametokana na utendaji kazi mzuri wa Mganga mkuu wa mkoa pamoja na timu yake RMO,kwani kwa kipindi cha miezi sita mapato yameongezeka kwa asilimia 300. "Nimesaini mkataba wa utendaji kazi kati yangu na  Wakuu wa wilaya .Niwapongeze  wakuu wa Wilaya kuwa sasa tunasomana" amesema Kafulila.

 Akiwasilisha taarifa ya hali ya utekelezaji mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 mkoa wa Simiyu,Kaimu Katibu Tawala M,Injinia Mashaka Luhamba alieleza kuwa Mkoa wa Simiyu umetengewa jumla ya Tshs 20,476,951,633.30 kwa ajili ya kutekeleza miradi inayolenga kuimarisha miundombinu ya Sekta za Elimu na Afya na mapambano dhidi ya UVIKO 19. Fedha hizo zimetolewa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Shule za Sekondari,Shule Shikizi,Hospitali za Wilaya katika ngazi za Halmashauri za Wilaya, Miji ,Manispaa na Majiji. Aidha, fedha zingine zimepelekwa kutekeleza miradi ya kipaumbele katika Hospitali ya Rufaa za Mkoa na Mamlaka za maji.

Kuhusu miradi ya ujenzi wa shule mkoani Simiyu,Injinia Luhamba amesema, hadi sasa miradi iliyoanza kutekelezwa ni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 380 vya shule za Sekondari na vyumba vya madarasa 69 vya Shule Shikizi. Mpaka sasa ujenzi huo umefikia  85% ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.Injinia Luhamba ameeleza kuwa pamoja na mafanikio haya katika ujenzi wa Madarasa Mkoa umekuwa ukikabiliwa na  changamoto mbalimbali hususani katika Wilaya ya Maswa na Itilima ambapo changamoto kubwa imekuwa upatikanaji wa vifaa. Vifaa vya viwandani kama vile bati na saruji kuchelewa kufika katika maeneo husika hasa kwa Halmashauri ambazo zilitumia mfumo wa manunuzi ya pamoja. Bei ya vifaa kupanda ghafla mara tu miradi ilipoanza na hivyo kusababisha gharama ya mradi kuongezeka.Shule ambazo ziliomba kibali cha kuhamisha fedha kwenda katika maeneo mengine kwa ajili ya ujenzi zilichelewa kupata kibali na hivyo kusababisha kuchelewa kuanza kwa mradi.

Kuhusu sekta ya afya,mganga Mkuu Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniface Marwa, ameeleza kuwa kwa kipindi cha miezi tisa kumekuwa na mafanikio makubwa sana katika sekta ya afya Mkoani Simiyu.Awali kulikuwa na vituo vya afya 218 lakini sasa kuna vituo vya afya 221.Aidha upatikanaji wa dawa nao umeongezeka kufikia asilimia 91.

 Dkt. Marwa amesema mafanikio yote haya yamepatikana kutokana ushirikiano uliopo baina ya wafanyakazi wa Sekta ya Afya, uongozi bora toka kwa mkuu wa mkoa na menejimenti yake. DKt Marwa amemfahamisha Naibu Waziri kuwa moja ya siri kubwa ya mafanikio haya ni usainishaji wa mikataba ya ya utendaji kazi katika sekta ya afya kati ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya ambao nao walisainishana na maafisa tarafa, Katibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri zote ambao nao wamesainishana na waganga wakuu wa halmashauri.

"Lengo la kusaini mikataba hii ni kuhakikisha utendaji kazi katika sekta ya afya unafanyika kwa weledi zaidi. Aidha ripoti za utendaji kazi zimekuwa zikitolewa kila robo mwaka na kwa kweli kumekuwa na mafaniko makubwa sana.Lengo letu ni kutaka kuwe na usimamizi na utendaji wa pamoja katika mkoa"amesema.Dkt Marwa.

 Akijibu hoja kuhusu changamoto ya uhaba wa watumishi sekya ya afya Mhe. Dugange amekiri kuwa mkoa wa Simiyu ni mmoja kati ya mikoa inayokabiliwa na changamoto  kubwa ya uhaba wa Watumishi wa  sekta ya afya.Serikali imeliona hilo na  inafanyia kazi kwa  kuendesha zoezi la kujua daktari na N esi ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wanaopaswa kuhudumiwa na dakkati /nesi mmoja ( Doctor/Nurse Patient ratio).Lengo la Serkali ni kuhakikisha kuwa kila mkoa uwe na watumishi angalau si chini ya  60% ya mahitaji yao .Akizungumzia 40% ya mapato ya ndani baada ya kutoa mapato lindwa, Mhe. Dugange amesema kuwa lazima fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo.

 Mhe. Festo Dugange yupo ziara Mkoani Simiyu kwa lengo la kupitia miradi ya ujenzi wa madarasa ya Uviko na vituo vya afya,ili kuona shughuli zinazoendelea na Changamoto mbalimbali wanazokalibiana nazo katika utekelezaji wa shughuli hizo. Mwisho

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa