Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha wanawalipa Madiwani stahili zao zote wanazodai kabla ya kuvunjwa kwa mabaraza ya Halmashauri ambayo yanatarajiwa kuvunjwa kabla ya tarehe 10 Juni 2020.
Mtaka ametoa agizo hilo Mei 26, 2020 katika kikao cha baraza maalum la Madiwani wilayani Busega ambacho kimefanyika kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
"Waheshimiwa madiwani wamefanya kazi nzuri kwa miaka mitano haitakuwa busara wamalize muda wao wakiwa wanadai; nisingependa kuona baada ya mabaraza kuvunjwa madiwani waanze kwenda kwenye ofisi za wakurugenzi kufuatilia madai yao, malipo yao yawe ndiyo kipaumbele cha Wakurugenzi wetu" alisema Mtaka.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya ameahidi kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa na kuhakikisha madiwani wote wanalipwa madai yao kwa wakati.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Imalamate, Mhe. Richard Magoti amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuliweka suala la malipo ya stahili za madiwani katika mkoa wa Simiyu kuwa kipaumbele, jambo ambalo limeonesha namna Serikali inavyothamini na kutambua mchango wa viongozi hao.
Naye Mbunge wa Busega Dkt. Raphael Chegeni amesema pamoaj na maendeleo yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano katika wilaya ya Busega wilaya hiyo inakabiliana na changamoto ya upungufu wa miundombinu ya elimu kutokana na ongezeko la wanafunzi, hivyo akatoa wito kwa Serikali kushirikiana na jamii kuona namna ya kukabiliana na changamoto hiyo.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/05/mkuu-wa-mkoa-wa-simiyu-mhe.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa