• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Halmashauri ya Maswa yashauriwa Kuwekeza katika Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi ili Kizalishe kwa Tija

Posted on: February 1st, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imeshauriwa kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi ikiwemo viatu, mikoba na mikanda kinachomilikiwa na kikundi cha Usindikaji Ngozi Senani kilicho kata ya Senani wilayani Maswa, ili kuongeza thamani ya ngozi zitokanazo na mifugo.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda vidogo katika wilaya MASWA.

Mtaka amesema katika kutekeleza Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda , Halmashauri ya Maswa inapaswa kuwekeza katika viwanda vinavyoanzishwa na vikundi ili kuviwezesha katika upatikanaji wa malighafi ya kutosha, kuongeza thamani ya mazao ya mifugo pamoja na kilimo ili viwanda hivyo viweze kuzalisha kwa tija.

“Tungehitaji kuwa mkoa ambao utawekeza sana katika viwanda vidogo na ndiyo maana tulianza dhana ya Wilaya moja bidhaa moja kiwanda kimoja na sasa tunakwenda kwenye Kijiji Kimoja Bidhaa Moja Kiwanda kimoja; tunataka kupunguza uagizwaji wa bidhaa kutoka nje ya Mkoa” alisema Mtaka.

Aidha, ameitaka Halmashauri hiyo kuwasaidia wanakikundi kuweka mifumo mizuri ya kutengeneza soko la bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kuuza katika minada yote ya wilaya hiyo na kuimarisha soko la nje.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko amesema Halmashauri itahakikisha kiwanda hicho kinapata  malighafi ya kutosha ambapo amebainisha kuwa Halmashauri imeingia mkataba na Chuo cha DIT Mwanza kuhakikisha kuwa inazalisha malighafi(ngozi) kwa wakati kwa ajili ya kiwanda hicho.

Akiwa Malampaka ambapo alitembelea Mradi wa Ghala na Mashine ya kukoboa mpunga na kupanga madaraja, Mtaka amekipongeza Chama cha Ushirika Bumala AMCOS kwa kuanzisha kiwanda, huku akiwataka wananchi  wa eneo hilo kujiandaa kiushindani katika biashara, kwa kuwa hivi karibuni Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa bandari ya nchi kavu itakayoenda sambamba na ujenzi wa Reli ya Kisasa(Standard Gauge).

“Ni lazima mjiandae kiushindani katika biashara, miaka mitatu ijayo katika Mipango ya Serikali Malampaka haitakuwa kama ilivyo, hapa ni mahali ambapo Standard Gauge ikianza bidhaa zitakuwa zikisafirishwa kwa wingi; nimeshaongea na Mkurugenzi kuwa eneo hili lipimwe na Halmashauri imiliki eneo la uwekezaji” alisisitiza Mtaka.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka alitembelea eneo la ujenzi wa  kiwanda cha kutengeneza ungalishe katika Kijiji cha Njiapanda, ambacho kitamilikiwa na shule 30 za Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, kinachoanzishwa kwa lengo la kuongeza kipato cha shule na halmashauri, kutoa ajira kwa wananchi na kuboresha lishe za watu.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa  wa Simiyu, Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Maswa, Mwl. Mabeyo Bujimu amesema shule za msingi 30 wilayani humo zitanufaika kwa kulima viazi lishe na kukiuzia kiwanda hicho kama malighafi pamoja na kuuza bidhaa zitakazozalishwa na kiwanda.

Huu ni mwanzo wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ambayo amepanga kutembelea viwanda vidogo vilivyopo katika wilaya zote za mkoa huo.

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII:BOFYA HAPA:https://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/halmashauri-ya-maswa-yashauriwa.html

MWISHO

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa