• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Darasa la Saba, Kidato cha Nne Simiyu Waahidi Kufuata Nyayo za Kidato cha Sita Kubaki Tatu Bora Kitaifa

Posted on: August 24th, 2020

Wanafunzi wa Darasa la Saba na Kidato cha nne Mkoani Simiyu wameahidi kufuata nyayo za kidato cha Sita kuendelea kufanya vizuri katika mitihani yao ya Kitaifa na kubaki katika nafasi tatu bora Kitaifa kama walivyofanya Kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa umekuwa wa tatu kati ya mikoa 29.

 Hayo yamesemwa na baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Somanda (B ) na kidato cha nne kutoka Shule ya sekondari Simiyu (Bariadi) waliowawakilisha wenzao katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita iliyofanyika24 Agosti 2020 Mjini Bariadi

“Tunawapongeza dada na kaka zetu  kidato cha sita kwa kufanya vizuri kwenye mtihani wao wa taifa tunaahidi kufanya vizuri kama wao;Shule yetu ya msingi Somanda B ina mkakati wa kuingia katika shule kumi bora kitaifa na kutoa wanafunzi wanne katika wanafunzi kumi bora Kitaifa,tunaahidi hatutawaangusha,”alisema Ezra Paulo mwanafunzi wa darasa la saba Somanda.

“ Matokeo ya Kidato cha Sita yametuhamasisha kujipanga zaidi kwa mwaka 2020, kupitia fursa mbalimbali ambazo tunapewa na viongozi wetu zikiwemo kambi za kitaaluma tunapata fursa ya kujisomea zaidi kuliko tukikaa majumbani, tunaahidi kufanya vizuri zaidi ya dada na kaka zetu walivyofanya ikizingatiwa kuwa shule yetu inabeba jina la mkoa,” Sarah Ndamo kutoka Simiyu Sekondari.

Kwa upande wake mwanafunzi Benard S. Benard kutoka shule ya sekondari Binza wilayani Maswa ambaye amepata daraja la kwanza pointi nne, amewaasa wanafunzi wenzake kuongeza bidii katika masomo kushirikiana na kuutumia vizuri muda wanaokuwa shuleni ili waweze kufikia malengo yao.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Bariadi, Mwl. Ally Simba amesema siri kubwa ya wanafunzi wa shule hiyo kufanya vizuri zaidi na kuifanya kuwa ya kwanza kimkoa na ya 24 Kitaifa ni kufanya mitihani ya mara kwa mara huku akibainisha kuwa wamejipanga kuwa katika shule kumi bora Kitaifa na kuibadilisha shule hiyo ili iwe miongoni mwa shule maalum nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga amesema siri kubwa ya kufanya vizuri ni mikakati iliyowekwa na mkoa pamoja na utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujiamini huku akisisitiza kila mdau atimize wajibu wake ili mkoa uendelee kufanya vizuri.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema mkoa umetimiza azma yake ya kutoka nafasi ya 10 mwaka 2019 na kuingia nafasi ya  tatu Kitaifa mwaka 2020 na kuongeza ufaulu kutoka GPA ya 3.0443 kufikia  2.894; huku akishauri kuwa ili Simiyu iendelee kufanya vizuri zaidi ni vema  ufundishaji makini uimarishwe zaidi..

Jumla ya wanafunzi 955 walisajiliwa kufanya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2020 mkoani Simiyu, kati yao wanafunzi watano hawakufanya mtihani na katika wanafunzi 950 waliofanya mtihani, wanafunzi 208 wamepata daraja la kwanza,  507 wamepata daraja la pili, 228  daraja la tatu,  wanafunzi 06 wamepata daraja la nne  na mmoja amepata daraja sifuri.

Pamoja na kutoa shilingi laki moja kwa kila alama A iliyopatikana kwenye somo lake mwalimu aliyefanya vizuri,wanafunzi wawili waliopata daraja la kwanza pointi nne wamepewa shilingi laki mbili kila mmoja;  Mkoa pia umetambua mchango wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  katika kukuza sekta ya elimu kwa kumtunuku cheti.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/08/darasa-la-saba-kidato-cha-nne-simiyu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa