• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Daktari Bingwa awatahadharisha Wananchi Kutochanganya Dawa za Hospitali na Kienyeji

Posted on: April 19th, 2019

Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani na maradhi ya moyo kutoka Wizara ya afya Prof. Harun Nyagori ametoa wito kwa Watanzania kutochanganya dawa za hospitali na kienyeji wakati wa matibabu yao ili kuepuka athari kubwa za kiafya zinazoweza kujitokeza.

Prof Nyagori ameyasema hayo Aprili 18, 2019  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano Mkuu wa chama cha wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE),unaofanyika mjini Bariadi.

Amesema kuwa uchanganyaji wa dawa za hospitali na za kienyeji ni hatari kwa afya ya binadamu, hivyo ni vema wagonjwa mbalimbali wa magonjwa ya ndani na maradhi ya moyo kuamua kufanya maamuzi ya matumizi ya dawa upande mmoja ili wasije kujisababishia madhara makubwa zaidi.

“Ni vema wagonjwa wasichanganye dawa za hospitali na za kienyeji, japo dawa nyingi za hospitali zinatengenezwa na Mitishamba lakini utofauti wa dawa za hospitali na dawa za kienyeji ni kwamba wanapotumia dawa za kienyeji wanatumia pasipokujua kiwango cha kemikali zilizopo na aina ya sumu iliyopo kwenye dawa hizo”

“Nimeona wagonjwa wengi wanaochanganya dawa za hospitali na za kienyeji wanapata madhara mbalimbali mwilini, wengine figo zao zimeshindwa kufanya kazi vizuri, wengine maini yameharibika, sukari imezidi kupanda; kwa hiyo nawashauri kama wakiamua kutumia dawa za hospitali watumie hizo na kama wameamua kutumia mitishamba wazitumie hizo tu wasichanganye” alisema Dkt. Nyagori.

Sambamba na hilo Prof Nyagori, pia amesema kuwa katika siku sita za mkutano mkuu wa ATAPE unaoendelea Mkoani Simiyu, ametoa wito kwa wananchi na wakazi wa Simiyu kujitokeza kwa wingi kupima afya zao.

Ameongeza kuwa ndani ya siku mbili ambazo wamekuwa wakitoa huduma hizo za magonjwa ya ndani na maradhi ya moyo, jumla ya wagonjwa 269 walijitokeza kupima afya zao na kati ya hao 103 waligundulika kuwa shinikizo la damu,62 walikuwa na sukari na 140 wenye uzito uliopindukia.

Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima afya zao wameshukuru huduma hizo kutoka kwa madaktari bingwa kusogezwa karibu yao kupitia mkutano wa ATAPE huku wakieleza kufurahishwa na huduma hizo kutolewa kwa gharama nafuu.

“Binafsi nimefurahishwa na huduma za madaktari bingwa ambazo nimezipata kupitia mkutano huu wa ATAPE, nimepima na nimeweza kujua afya yangu, kilichonifurahisha zaidi ni kwamba nimetumia shilingi elfu kumi tu kupima shinikizo la damu, sukari na vipimo vingine”alisema Mchungaji Marco Barnabas.

“Huduma zinazotolewa hapa ni nzuri na zinatolewa kwa gharama nafuu kabisa nitoe wito kwa Wanasimiyu kujitokeza kwa wingi kuja kupima afya zao, ili waweze kutambua hali za afya zao na kupata ushauri wa wataalam bingwa” alisema Namkunda Mburuja.

Mkutano Mkuu wa Mkuu wa chama cha wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE),unaendelea  mjini Bariadi na unatarajiwa kuhitimishwa Jumapili ya tarehe 21/04/2019; wanataaluma mbalimbali wanaendelea kutoa huduma, huku wajasirimali wakiendelea kuuza bidhaa mbalimbali katika viwanja vya shule ya Sekondari Kusekwa memorial

MWISHO

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa