• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

CWT Tegueni Kitendawili cha Walimu Kukopa Nje ya Mfumo Rasmi: RC Mtaka

Posted on: October 31st, 2019

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) kuja na majawabu ya kuwasaidia walimu kuacha kukopa katika taasisi za fedha zisizo rasmi ambazo hazijasajiliwa na wafanyabiashara binafsi ambao wamekuwa wakichukua kadi zao za benki (ATM) na kukaa nazo na kuwatoza riba kubwa.

Mtaka ameyasema hayo katika Mkutano wa ujirani mwema wa Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) ulioshirikisha viongozi kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera, Mkutano uliofanyika Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

Amesema ni vema walimu wabadilike na kutumia taasisi rasmi za fedha kuchukua mikopo badala ya kukopa kwa wafanyabiashara binafsi au taasisi za fedha zisizo rasmi(ambazo hazijasajiliwa) ili waondokane na mikopo inayowaumiza kwa kuwa na riba kubwa.

“ Kuna wafanyabiashara wanakaa na kadi za ATM za walimu wetu, wakati  mshahara unapotoka wanaenda kuchukua fedha na wanabaki na hizo kadi, ni lazima CWT mje na majawabu ya kuwasaidia walimu wanaokopa nje ya mfumo wa kibenki usio rasmi kwa sababu CWT sasa hivi ina benki; vilevile Benki kuu, benki zote za biashara na HAZINA wana utaratibu wa mikopo kupitia mishahara yetu,” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka ameahidi kuwa katika Mkoa wa Simiyu, Viongozi wote watahakikisha wanawapa kipaumbele na hawatakuwa tayari kuona watumishi wa kada nyingine wakiwadhalilisha walimu

Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenyeulemavu, Mhe.Stella Ikupa amewapongeza Chama cha Walimu kwa kuwajumuisha watu wenye ulemavu katika ngazi za uongozi na kusisitiza walimu kupata mafunzo ya elimu maalum  ili waweze kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum waliopo katika shule zao.

“Niwapongeze CWT kujumuisha walemavu katika uongozi pia iwapongeze walimu wote kwa kazi kubwa mnayofanya, mna mchango mkubwa kwa ustawi wa mtu mmoja mmoja, kada mbalimbali na jamii kwa ujumla, Serikali imeendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali za walimu, ikiwemo kuwapandisha madaraja ambapo hivi karibuni walimu 124,000 walipandishwa madaraja,” alisema Ikupa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema Serikali imehakikisha wananchi wanapata taarifa kwa wakati, hivyo imetungwa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa mwaka 2016, ili kuruhusu kila mwananchi kufahamu mambo mbalimbali yanayoendelea kuhusu utendaji wa Serikali.

Ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kufanya mageuzi makubwa kiuchumi, ndio maana kuna utekelezaji wa miradi mikubwa kama mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere, na mradi wa reli ya kisasa, huku akibainisha kuwa pia  Serikali inaendelea kununua ndege, kwa sababu ndege ni uchumi na zinasaidia kukuza sekta ya utalii nchini.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Taifa, Mwl. Deus Seif amesema walimu wataendelea kuchapa kazi huku akiomba Serikali kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kutopandishwa madaraja na mishahara kwa wakati, malipo ya fedha za likizo, uhamisho na malimbikizo ya mishahara.

Akichangia hoja katika mkutano huo Kiongozi wa CWT kutoka wilayani Misungwi Mwanza, Mwl Rosemary Mboneko ameiomba Serikali iwasaidie walimu wanaoomba uhamisho kuwafuata wenza wao waruhusiwe ili kuepuka ndoa za masafa na kuwafanya watumishi hao wakafanya kazi kwa amani.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/11/cwt-tegueni-kitendawili-cha-walimu.html

 

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa