Taasisi nyingi ambazo zimekuwa zikipata fedha kupitia ushuru wa Pamba, zimeshindwa kuwasadia wakulima na badala yake wanaonufaika ni viongozi kupitia fedha zinazotokana na Pamba ya wakulima.Hali hii imepelekea wakulima wengi nchini wakiwemo wanaozalisha Pamba, kuchukia ushirika licha ya kulazimishwa kupeleka mazao yao Amcos kwa ajili ya kuuzwa.
Mhe. Kafulila amesema hayo, wakati wa kikao na viongozi wa vikozi kazi vya zao la Pamba alipotembelea Tarafa ya Mwamapalala Wilaya ya Itilima. Mhe. Kafulila amesema Bodi ya Pamba, Vyama vya msingi vya Ushirika (Amcos), SIMCU ni vyombo ambavyo vinatakiwa kusimamia zao la Pamba na kuwasaidia wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija.Vyombo hivyo vimekuwa vikikusanya ushuru unaotokana na zao la Pamba ambalo ni jasho la mkulima, lakini wameshindwa kuwasaidia wakulima.
“Kwa mkoa wa Simiyu, msimu uliopita Amcos walipata zaidi ya Bilioni 4, Chama kikuu cha ushirika (SIMCU) walipata zaidi ya Milioni 800, Bodi ya Pamba nayo ilipata fedha nyingi, lakini fedha hizo hazijarudi kwa wakulima kuwasaidia,”alisisitiza Kafulila.
Msingi wa kuanzishwa kwa vyombo hivyo,ulikuwa kukusanya ushuru na baada ya msimu kuisha kuwasaidia wakulima wakati wa maandalizi ya msimu mpya ili kuweza kuzalisha kwa tija.
“ Kama mkoa tumeanza kupambana na hii mifumo kwa kuifanyia marekebisho, tumeanza na hii ya mkulima kuwa mwanachama, tunataka kila mkulima awe mwanachama kwa sharti la kumiliki shamba la pamba,”amesema Kafulila.
Tumepeleka mapendekezo Wizara ya Kilimo, kubadilishwa kwa masharti ambapo mkulima kigezo cha kujiunga na Amcos kitakuwa shamba lake na siyo vigezo vingine vilivyopo kwa sasa ikiwemo pesa. Hali hii itafanya wakulima kuongezeka kwenye Amcos na maamuzi kufanywa na wengi, lakini pia kuweza kupata viongozi sahihi na siyo kama ilivyo sasa ambapo wanachama ni wachache na wanafanya maamuzi ya wakulima wote.
Hata hivyo Kafulila ameeleza kuwa mbali na hilo kama mkoa watapitia mifumo yote na kuhakikisha inabadilishwa ndani ya mkoa, ambao umejiwekea lengo la kuzalisha tani laki tano katika msimu ujao wa Pamba 2021/22..
|
|
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa