• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Bilioni 375.4 Zatolewa kutekeleza Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi na Kutatua Tatizo la Maji Simiyu

Posted on: November 29th, 2017

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani, Mfuko wa Mabadiliko tabia nchi (CGF) na wananchi, imetenga kiasi cha shilingi bilioni 375.4 kutekeleza Mradi wa kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi mkoani SIMIYU kwa awamu ya kwanza, ambao utakuwa suluhisho la kudumu la tatizo la maji mkoani humo

Hayo yamesemwa leo  na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe wakati akifungua kikao cha wadau wa mabadiliko ya tabia nchi kilichofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Waziri Kamwelwe amesema moja ya shughuli muhimu na kubwa katika utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi,  ni ufikishaji wa huduma ya Maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Bariadi , Busega na Itilima kwa awamu ya kwanza na baadaye katika Wilaya ya Meatu na Maswa.

Ameongeza kuwa upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Simiyu uko chini ikilinganishwa na wastani wa Kitaifa na kwa kutambua hali hii,  Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ilibuni mradi huu,  ili kupata suluhisho la kudumu  la tatizo la maji kwa wananchi na mifugo ambayo ni moja ya shughuli za kiuchumi za wananchi wa Mkoa wa Simiyu.

Aidha, Waziri Kamwelwe amesema lengo la mradi huu ni kuboresha Afya na kuongeza uzalishaji maji ili kuinua hali ya maisha kwa wananchi walioathirika na mabadiliko ya tabia nchi, ambapo amebainisha kuwa katika kufikia lengo shughuli mbalimbali zitatekelezwa katika nyanja za maji safi na usafi wa mazingira, kilimo endelevu na ufugaji.

Waziri pia amebainisha kuwa kutakuwa na ujenzi wa mabwawa ya kilimo cha umwagiliaji endelevu na maji ya mifugo, ujenzi wa mabwawa ya kutibu maji taka pamoja na  vyoo vya mfano katika Shule na Vituo vya Afya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo ambao utawasaidia wananchi wa mkoa huo na utakuwa chachu katika Ujenzi wa Viwanda mkoani humo kwa kuwezesha upatikanaji wa maji ya uhakika.

“Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wote wanausubiri sana mradi huu wa maji ya Ziwa Victoria; pia Mkoa wetu unaenda kwenye uwekezaji wa viwanda vikubwa na changamoto tuliyonayo ni suala la upatikanaji wa maji ya uhakika, utekelezaji wa mradi huu utatusaidia sana katika viwanda” amesema Mtaka.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa Simiyu ni Miongoni mwa Mikoa yenye kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma ya maji ambayo Serikali imetoa kiupaumbele cha kuipa fedha kutoka katika Fedha za Mfuko wa Maji ili kutekeleza miradi ya maji itakayoibuliwa na kuwasilisha maandiko yake wizarani.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amewahimiza Wataalam wa Halmashauri kwa kushirikiana na Mkoa kuandaa maandiko ya kuibua miradi ya Maji itakayowasilishwa wizara ya maji,  kwa lengo la kuomba fedha za  kutekeleza miradi hiyo ili kuongeza na kuboresha upatikanaji wa huduma za maji mkoani humo.

Mradi wa kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi Mkoani SIMIYU ambao zabuni yake imepangwa kutangazwa Januari 2018; utatekelezwa kwa awamu mbili awamu ya kwanza utaanza na Mji wa Bariadi, Busega na Itilima pamoja na vijiji 278 vilivyopo pembezoni mwa bomba kuu umbali wa Kilomita 12 kila upande,  baadaye maeneo mengine ya Wilaya za Maswa na Meatu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wadau wa Mradi wa  kukabiliana na changamoto zitokanazo  na Mabadiliko ya Tabianchi (hawapo pichani) unaotekelezwa Mkoani humo, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na  Wadau wa Mradi wa  kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi (hawapo pichani) unaotekelezwa Mkoani Simiyu  kwenye kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa Mradi wa  kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi, unaotekelezwa Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.

Baadhi ya wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi  unaotekelezwa Mkoani Simiyu akifuatilia masuala mbalimbali yalikuwa yakijadiliwa katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.

Baadhi ya wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi  unaotekelezwa Mkoani Simiyu akifuatilia masuala mbalimbali yalikuwa yakijadiliwa katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.

KWA PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILI BOFYA HAPA CHINI

https://simiyuregion.blogspot.com/2017/11/bilioni-3754-zatolewa-kutekeleza-mradi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa