Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe. Prof. Dkt..Ratlan Pardede na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla Agosti 04, 2019 wametembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea wageni hao Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema asilimia 80 ya uchumi wa nchi unategemea kilimo, hivyo kwa kuwa Mhe.Kigwangalla ni Waziri mwenye Dira kwa kutembelea maonesho haya atatoa mchango,mawazo na hamasa kubwa kuhusiana na sekta ya kilimo.
Aidha, amesema Prof.Dkt.Ratlan Pardede amekuja kwa mara ya pili sasa Mkoani Simiyu, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Indonesia na Mkoa wa Simiyu (Tanzania.)
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Dkt.Hamisi Kigwangalla amepongeza waandaji wa maonesho haya ya Nanenane Kitaifa (Kanda ya Ziwa Mashariki) kwa maandalizi mazuri ya pia amewapongeza Wakulima na Wafanyabiashara kwani kwa kushiriki maonesho haya wanapata fursa ya kujifunza na kuuza mazao yao.
Amesema sekta ya kilimo ni sekta muhimu kwani ndiyo sekta inayoajiri wananchi wengi ikifuatiwa na sekta ya utalii na inategemewa na Uchumi wa Viwanda kutoa malighafi za viwanda, huku akibainisha kuwa Utalii unachangia pato la Taifa kwa asilimia 17.6 , pia unachangia kwa zaidi ya 25% ya upatikanaji wa fedha za kigeni.
.
Mhe. Kigwangalla ameongeza kuwa mwaka 2015 kulikuwa na ongezeko la Watalii kutoka Milioni 1 hadi milioni 1.1, .Mwaka 2018 Watalii waliongezeka hadi kufikia Milioni 1.6 na lengo likawa ni kufikia mwaka 2020 idadi iongezeke zaidi na kufikia watalii milioni mbili.
Naye Balozi wa Indonesia Prof.Dr.Ratlan Pardede amesema amefurahi kufika Mkoani Simiyu kwa mara ya pili sasa na Indonesia inashiriki Maonesho ya Nanenane ili kuimarisha uhusiano wake na Tanzania hususani katika kilimo.
“Nimefura sana kufika kwa mara ya pili sasa mkoani Simiyu tunashiriki Nanenane kwa sababu tunataka kuimarisha uhusiano wetu na Mkoa wa Simiyu hususani katika kilimo, kusudi likiwa ni kuona kwa jinsi gani tunaweza kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika siku za usoni kwa manufaa ya nchi zote mbili yaani Tanzania na Indonesia” alisisitiza.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/08/balozi-wa-indonesi-waziri-kigwangalla.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa