• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Balozi Kazungu: Ningependa Nione Takwimu Za Biashara, Uwekezaji Kati Ya Tanzania Na Kenya Zikiongezeka

Posted on: October 6th, 2018

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu amesema angependa kuona  katika kipindi chake atakachokuwepo hapa nchini akiiwakilisha nchi ya Kenya ushirikiano wa kiabishara katika Kenya na Tanzania na unaimarika na takwimu za biashara, viwanda na uwekezaji kati ya nchi hizo zikiongezeka mara dufu.

Balozi Kazungu ameyasema hayo wakati alipotembelea Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery LTD), kilichopo Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Oktoba 05, 2018 katika ziara yake mkoani Simiyu.

Balozi Kazungu amesema ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hususani katika viwanda, kati ya Tanzania na Kenya ukiendelea kuimarika zaidi utachangia kuongeza ajira, kuwatoa wananchi katika umaskini pamoja na kuimarika kwa uchumi wa nchi hizo pia.

 “Baada ya miaka minne kazi yangu kama ikiisha hapa, naomba nione takwimu za viwanda, biashara, uwekezaji kati ya Tanzania na Kenya zinaongezeka mara dufu, nafasi za kazi kwa watu wetu zinapatikana na watu wetu wanaondokana na umasikini; kukua kwa Tanzania kuwe ndiyo kukua kwa Kenya hilo ndiyo ombi letu” alisema Mhe. Balozi Kazungu.

Aidha, Mhe. Kazungu ametoa wito kwa  wananchi wa Tanzania na Kenya kuepuka migogoro ya kibiashara ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kuchangia katika kushuka kwa biashara kati ya nchi hizo, huku akiwataka waandishi wa habari kuwa makini na kijiridhisha kabla kuandika habari za kibiashara kwani zisipoandikwa kwa usahihi zinaweza kuchochea migogoro ya kibiashara.

Aidha, Balozi Kazungu amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kuwa atakuwa mstari wa mbele kuzungumza na wawekezaji nchini Kenya ili waje kuwekeza, ambapo amebainisha kuwa Sekta binafsi na Shirikisho la watu wenye viwanda hapa nchini wameshaanza kuzungumzia masuala hayo na wenzao wa Sekta binafsi Kenya.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka amemwomba Balozi Kazungu kuwaalika wawekezaji kutoka nchini Kenya na kubainisha kuwa mkoa uko tayari kutoa ardhi bure kwa wawekezaji watakaojenga viwanda vinavyojibu mahitaji ya mkoa, hususani katika kuongeza thamani ya zao la pamba, mazao yatokanayo na mifugo kama ngozi na nyama.

Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu una uwezo wa kuzalisha pamba zaidi ya kilo milioni 400 na hadi sasa umezalisha kilo milioni112 ambazo ni zaidi ya asilimia 50 ya pamba yote nchini; hivyo katika kuiongezea thamani pamba hiyo kiwanda kikubwa cha kuzalisha bidhaa zaidi ya 20 za afya zitokanazo na pamba

“Simiyu tunao uwezo wa kuzalisha zaidi ya kilo milioni 400 za pamba, mpaka sasa tumezalisha kilo milioni 112 ambazo ni zaidi ya asilimia 50 ya pamba yote inayozalishwa hapa nchini; katika kuongeza thamani ya zao la pamba, mwaka huu tutaanza ujenzi wa kiwanda kikubwa kitakachozalisha zaidi ya bidhaa 20 za afya zitokanazo na pamba, kitakachojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kwa kushirikiana na wadau wengine na Mkoa wa Simiyu tumetoa ardhi bure” alisema Mtaka.

 Ameongeza kuwa kipaumbele cha pili cha mkoa baada ya kujenga kiwanda hicho ni kuwa na uwekezaji katika viwanda vya nguo(textile industries) ili kupata bidhaa ya mwisho katika zao la pamba, hivyo akaendelea kutoa wito kwa wawekezaji ndani na nje ya nchi kuwekeza katika eneo hili.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni Mwekezaji kutoka Nchini Kenya amesema lengo la Kampuni hiyo yenye Kiwanda cha kuchambua pamba ni kwenda katika kuongeza thamani ya zao la pamba, ili faida itakayopatikana irudi kwa wakulima kwa kuifanya pamba yao ikanunuliwa kwa bei nzuri itakayowapa motisha ya kuendelea kuzalisha zaidi.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KINGANISHI HIKI:-


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa