• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Askofu Sangu Awataka Vijana Wasikubali Kutumiwa Kuleta Chuki, Fitina na Mafarakano

Posted on: September 3rd, 2017

Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu amewataka Vijana kutokubali kutumiwa kuleta vurugu, chuki na mafarakano hapa nchini.

Askofu Sangu ametoa wito huo wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

“......Maandiko Matakatifu yanasema Vijana wana nguvu;  kwa hiyo nawasihi vijana popote pale mlipo muwe chimbuko la Upendo, furaha na amani; watu wengine wasitumie nguvu zenu vijana kuleta chuki, fitina na mafarakano, muwe macho” alisema Askofu Sangu.

Askofu Sangu amewaasa waumini wa Kanisa hilo kuishi maisha mema ambayo hayatakuwa chanzo cha mateso kwa watu wengine katika familia, jumuiya , jamii wanaoishi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, amewataka Watanzania wote kupinga na kukemea mauaji ya watu wenye ualbino kwa kuwa wanayo haki ya kuishi kama watu wengine na watu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa Kanisa kuwa na mtazamo wa  kuisaidia nchi katika kupambana na tatizo la ajira hususani  kwa vijana.

Ameongeza kuwa ni vema Kanisa liyavae maneno ya Mhe.Rais kuhusu Ujenzi wa Tanzania ya Uchumi wa Kati na kuona namna linavyoweza kushiriki katika kufikia Tanzania Mpya, kwa kuimarisha Idara za Kanisa na Vyama vya Kitume na kuzijenga idara na vyama hivyo katika mtazamo wa Kiujasiriamali.

 “Kanisa lione namna gani WAWATA tulionao wanakuwa WAWATA wa miradi, VIWAWA wanakuwa wa miradi, TYCS wa miradi, lakini sasa Vyama vyetu vya Kitume navyo pia vianze kujielekeza kusaidia Kanisa kwenye eneo la miradi”amesema Mtaka.

Mtaka amesema upo umuhimu wa kufanya semina za Ujasiriamali kwa vijana, wanawake na Vyama vya Kitume katika Kanisa  na waumini wote kwa ujumla ili kuwa na waumini waliojengwa kiuchumi na wanaoendana na mtazamo wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia Uchumi wa Kati.

Akiwa katika Ziara yake Mkoani Simiyu, Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu , Jumamosi Septemba 02 alizindua Parokia mpya ya Mtakatifu Luka iliyopo  Mjini BARIADI,  sambamba na kutoa kipaimara na leo ametoa kipaimara kwa vijana 164, katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiwapaka mafuta vijana wa Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika  katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Baadhi ya Vijana waliopata Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi wakiimba katika ibada .

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (mwenye shati jeupe) na Mkewe Neema Mbiha(kulia) wakifuatilia mahubiri wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi iliyoongozwa na Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa