• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

AMREF Watoa Msaada wa Vifaa Kinga kwa Ajili ya Tahadhari ya Corona Simiyu

Posted on: July 10th, 2020

Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF kupitia mradi wa UZAZI UZIMA limetoa msaada wa vifaa kinga kuunga mkono Serikali katika tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya CORONA kwa mkoa wa Simiyu.

Akikabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni 23, Mratibu wa AMREF Kanda ya Ziwa, Bw. Gaspery Misungwi amesema Shirika hilo linatambua kazi kubwa iliyofanywa na Serikali katika mapambano dhidi ya Corona hivyo kama wadau wameona waungane na serikali katika kutokomeza kabisa janga hilo.

Aidha, Bw. Misungwi amevitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na mmipira ya kuvaa mikononi wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa, barakoa,vitakasa mikono (ujazo tofauti), sabuni za maji za kunawia mikono(ujazo tofauti) na ndoo kwa ajili ya kunawia mikono.

Akipokea msaada huo, Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo huku akibainisha kuwa vifaa kinga hivyo havitatumika katika tahadhari dhidi ya corona peke yake maana utakasaji unazuia magonjwa mengi.

Mmbaga ameongeza kuwa mkoa wa Simiyu uko tayari kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau wote kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Serikali kwa kuwa nia ya serikali ni kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Mmbaga ameelekeza vifaa hivyo vipelekwe katika maeneo yaliyokusudiwa na wala visipelekwe stoo.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Khamis Kulemba amesema pamoja na AMREF kutoa vifaa kinga hivyo shirika hilo limekuwa likisaidia katika ujenzi wa miundombinu hususani majengo ya upasuaji katika baadhi ya vituo, uchimbaji wa visima Vya maji na katika huduma za afya ya mama na mtoto.

Dkt. Kulemba ameongeza kuwa kwa ushirikiano kati ya AMREF na serikali hali ya mahudhurio ya wakina mama wajawazito kuhudhuria kliniki imeongezeka kufikia asilimia 80 na wanawake kujifungulia katika vituo Vya kutolea huduma za afya.

MWISHO

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa