• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Aliyekuwa RAS Simiyu Amkabidhi Ofisi Mrithi Wake

Posted on: July 8th, 2020

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amemkabidhi rasmi ofisi mrithi wake Bi. Miriam Mmbaga ambaye aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Julai 03, 2020 kuchukua nafasi hiyo.

Makabidhiano hayo yamefanyika Julai 08, 2020 mjini Bariadi na kushuhudiwa na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa dini, wakuu wa mashirika na taasisi za umma na binafsi pamoja na watumishi.

Akizungumza kabla ya makabidhiano hayo Sagini amemshukuru Mhe. Rais kwa kumuamini na kumteua ili aweze kuwatumikia wananchi kwa nafasi ya Katibu Tawala wa Mkoa huku akiwashukuru viongozi, watumishi na wananchi wa mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote alichokuwepo Simiyu.

“Namshukuru sana Mhe. Rais kwa imani yake kwangu nakumbuka mwezi Desemba 2015 alipoteua Makatibu Wakuu, makatibu wakuu tisa tuliachwa tukapangiwe kazi nyingine lakini baada ya muda akaniteua kuwa katibu tawala wa mkoa, nakumbuka katika wale tisa ni mimi peke yangu ndiyo niliteuliwa kuwa katibu tawala wa mkoa; hii ni imani kubwa sana kwangu,” alisema Sagini.

Aidha, Sagini ametoa wito kwa viongozi, watumishi na wananchi na wadau mbalimbali wa mkoa wa Simiyu kumpa ushirikiano Katibu Tawala mpya wa mkoa kama walivyokuwa wanampa yeye ili aweze kutimiza wajibu na majukumu yake kama inavyotakiwa.

Wakizungumzia aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini viongozi wa serikali, chama, wakuu wa taasisi na watumishi wamesema Sagini alikuwa kiongozi na mwalimu wao katika utendaji kazi wao huku wakibainisha kuwa amewasaidia katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za kiutendaji.

“Sagini tumeshirikiana naye katika kipindi chote tulichokuwa pamoja naye, amefanya kazi iliyoacha alama kwenye mkoa hata zawadi alizopewa hapa ni moja ya alama za kazi yake nzuri, tunamtakia kila la heri; nitumie nafasi hii pia kumkaribisha RAS wetu mpya mimi na wenzangu tunakuhakikishia kukupa ushirikiano,” alisema Mhe. Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

“Binafsi kaka yangu Sagini alikuwa si kiongozi tu bali mwalimu  kwangu amenifundisha vitu vingi sana maana mimi nimefanya kazi muda mfupi sana serikalini, miaka mingi nimefanya kazi katika sekta binafsi na nilikuwa sijui mambo mengi , yeye ndiye aliyenielekeza namna sahihi ya kutekeleza majukumu yangu,” alisema Mkuu wa wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera.

“Tunampongeza ndugu yetu Sagini kwa namna alivyokiunganisha Chama Cha Mapinduzi na watendaji wa Serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa mawasiliano na mahusiano kati yetu sasa hivi yameimarika sana; pia nampongeza  kwa namna alivyokuwa mwepesi kushughulikia changamoto za watumishi, wananchi na viongozi wa chama alizokuwa anapelekewa,” katibu wa itikadi na uenezi CCM Mkoa wa Simiyu, Bw. Mayunga George.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amemshukuru Mhe. Rais kwa kumteua kushika nafasi hiyo huku akiahidi kushirikiana na wadau wote  kuendelea kuleta matokeo chanya katika mkoa ili uendelee kuwa mkoa bora ndani ya nchi na Afrika Mashariki na watu wengine wajifunze Simiyu.

Aidha, Bi. Mmbaga ametoa wito kwa watumishi kuzingatia nidhamu katika utumishi wao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu na kuwataka kila mmoja atimize wajibu wake huku akibainisha kuwa kila mtu akitimiza wajibu wake kero mbalimbali za wananchi zitatatuliwa na rasilimali za umma zitaokolewa.

Bw. Jumanne Sagini alikuwa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa pili tangu mkoa wa Simiyu uanzishwe mwaka 2012 na alikabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake Bi. Mwamvua Jilumbi Mei 02, 2016.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/07/aliyekuwa-ras-simiyu-amkabidhi-ofisi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa