Wananchi wa Vijiji vya Ikinabushu na Isuyu wilayani Bariadi wameishukuru Serikali kwa kuwajengea daraja ambalo limerahisisha mawasiliano na usafirishaji wa abiria, mazao na mizigo kutoka Ikinabushu-Isuyu-Dutwa-Bariadi na Lamadi.
Shukrani hizo zimetolewa mara baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kufungua daraja la Isuyu Mei 26, 2019
Wananchi hao wamesema kabla ya kujengwa kwa daraja hilo walikuwa wakitumia daraja la kamba na miti na kutozwa fedha.
“ Tunaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutuwezesha kupata daraja sasa hivi watoto wetu wanaenda shuleni kwa raha hata mvua ikinyesha, kabla ya kujenga daraja hili watu walikuwa wanahatarisha maisha” alisema John Maduhu.
“mvua ikinyesha ilikuwa shida kuvuka kwenda Dutwa maana tulikuwa tunatakiwa kuvushwa kwa kamba” alisema Ester Saguda.
Awali akikagua kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo kijiji cha Igaganulwa Kata ta Dutwa, Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali ametoa wito kwa Halmashauri na wawekezaji wengine kutoa kipaumbele kwa wataalam wazawa katika fursa za ajira ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa kati na kulitumikia Taifa.
Akiwasilisha taarifa kwa kiongozi huyo, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni kuunga mkono utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda kufikia uchumi wa kati na ni mradi wa kujipatia mapato ya ndani.
Ukiwa wilayani Bariadi Mwenge wa Uhuru umepitia miradi minane yenye thamani ya shilingi milioni 700.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/05/wananchi-waishukuru-serikali-kuwajengea.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa