• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wananchi Watakiwa Kujitokeza Kupima Bure Magonjwa Yasiyoambukiza katika Maonesho ya Nanenane Simiyu

Posted on: July 31st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujitokeza kupata huduma ya upimaji wa magonjwa yasiyaombukiza katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwenye Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane  yatakayofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mhe. Mtaka ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Maonesho la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lililopo Uwanja wa Nananenane kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Amesema NHIF itatoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya saratani ya mlango wa kizazi, saratani ya matiti, kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza bure , hivyo hii ni fursa wananchi wa mkoa huo kwa kuwa itawapunguzia gharama waitumie vizuri.

Wakati huo huoMtaka ametoa wito kwa wananchi mmoja mmoja na vikundi vikiwemo vyama vya ushirika zaidi ya 390 mkoani humo kujiunga nakuwa na kadi za Bima ya Afya,  ili waweze kuwa na uhakika wa kupata huduma wakati wowote na kupunguza gharama za matibabu.

“Mini naamini ugonjwa hauna hodi hivyo nitoe wito kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa bima ya afya na sisi kwetu bima ya afya ni kipaumbele kwa kuwa tunahitaji mapinduzi ya kuchumi na kielimu tunayofanya ndani ya mkoa yaende sambamba na watu kupata kadi za bima ya afya, ili waone thamani ya Serikali kuwekeza katika sekta ya Afya” alisema.

“Katika sherehe za nanenane za mwaka 2018 niwaombe wananchi popote walipo watumie fursa hii ya kufikiwa na wenzetu wa Bima ya Afya,ili wawezeka kupata huduma za upimaji magonjwa yasiyoambukiza bure na kujiunga na bima ya afya “ alisisitiza.

Naye Meneja Masoko na Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hilipoti Lello  amesema pamoja na kutoa huduma za upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza bure, huduma za usajili kwa ajili ya kupata kadi za bima ya afya  ya mtu mmoja , familia na vikundi zitatolewa ambazo zitalipiwa kulingana na aina ya kadi itakayotolewa .

“Tutatoa huduma za usajili na kutoa kadi za bima ya afya katika banda hili na mtu akishasajiliwa hapa kadi zitatolewa hapa hapa, tutakuwa na kadi za watoto toto afya kadi, tutakuwa na huduma za ktoa kadi kwa vikundi na kwa wakulima ni kwa wale walio kwenye vyama vya ushirika(AMCOS); mtu yeyote atakayepata kadi hii atapata matibabu Tanzania nzima kuanzia Zahanati hadi hospitali ya Rufaa” alifafanua.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa, Bw. Shabani Kiduta ametoa wito kwa Wananchi wa mkoa wa Simiyu kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza kujua afya zao na kupata tiba, ili Mapinduzi makubwa ya kiuchumi yanayofanywa mkoani humo yaweze kuwafikiwa wakiwa na afya njema.

MWISHO


KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSUHABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/07/wananchi-watakiwa-kujitokeza-kupima.html


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • Naibu Waziri Silinde Aridhishwa Ujenzi wa Bwalo, Madarasa Sekondari ya Anthony Mtaka Busega

    March 06, 2021
  • A NaibuWaziri Silinde Aridhishwa Ujenzi wa Bwalo, Madarasa Sekondari ya Anthony Mtaka Busega

    March 06, 2021
  • Naibu Waziri Silinde Atoa Miezi Miwili Bariadi, Itilima Kukamilisha Mabweni

    March 05, 2021
  • Bilioni 75 Kujenga Kituo Cha Kupozea Umeme Simiyu

    March 04, 2021
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa